GET /api/v0.1/hansard/entries/532233/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532233,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532233/?format=api",
"text_counter": 289,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwashetani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, historia ya watu wetu kunyang’anywa mashamba imekithiri. Zaidi ya mara tatu, tumeihusisha Tume ya Ardhi kwenye masuala ya mashamba ambayo yamechukuliwa. Lakini Tume hiyo bado haijatupatia mwelekeo wowote. Hivi sasa, hata wakazi wangu wa Lunga Lunga wanaoishi kwenye kipande cha ardhi chenye ekari 1,083 wanaondolewa. Nyumba zao zimeharibiwa na wataondolewa wakati wowote kutoka kwa mashamba hayo. Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) hukusanya fedha ambazo hutumika kutekeleza miradi ya Serikali. Kupitia Kamati ya Fedha, Mipango na Biashara, nilitaka kujua viwango vya ushuru wa VAT wanaotozwa wanabiashara wanaoingiza magari humu nchini, na jinsi ushuru huo unavyokusanywa. Lakini mpaka sasa, sijapata ripoti yoyote. Mwaka umepita sasa tangu nilipowasilisha ombi hilo. Kila siku nikiuliza swali hilo, napelekwa huku na kule. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}