GET /api/v0.1/hansard/entries/532595/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532595,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532595/?format=api",
    "text_counter": 63,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, leo twajadili kuhusu Hotuba iliyotolewa na Rais. Hotuba hii ni ya pili tangu Bunge la Seneti liundwe. Alisema mambo kadhaa na ilikuwa Hotuba ndefu ya maana na ilitukumbusha mambo mengi. Alitwambia mahali tunatoka na pale tunaenda. Pia, alisema kuwa uchumi wetu ulikuwa katika mwaka wa 2014 hadi kwamba ukigawanywa kwa kila mtu, unawezapata US$ 1,246. Sisi tena sio mkia wa nchi za uchumi, tuko katikati, tunasonga mbele. Leo Kenya inatambulika kama inayokua kiuchumi kwa kasi kwa asilimia sita, ikiwa nambari tisa kwa nchi za Africa. Alisema kwa nchi 57 ambazo zinakua kwa uchumi wa kasi ulimwenguni, Kenya inaodhoreshwa kwa namba tatu. Rais alisema kwamba nguvu za umeme zimesambaziwa wananchi kutoka asili mia 26 hadi asili mia 37 na, kwa hayo, yuastahili kupongezwa kwa sababu haya ni mambo yanayoashiria maendeleo. Rais pia alitaja mashule na ukuaji wa mashule. Pia, alitaja mambo ya utawala, barabara na mpango wa Lamu Port–South Sudan–Ethiopia Transport ( LAPPSET ) na tumefikia wapi hadi sasa. Rais pia alitaja mambo ya kusaidia The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}