GET /api/v0.1/hansard/entries/532597/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532597,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532597/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kutoa vifaa kwa hospitali zetu, mpango ambao Serikali itatumia hela nyingi ambapo karibu hospitali 94 katika kaunti 47 zitafaidika, na kwa hayo, twamshukuru. Bw. Naibu Spika, Rais pia alitukumbusha kwamba lazima tuwe wazalendo, lakini akalalamika kwamba ingawa anataja na kutoa mwito kuwa tuwe wazalendo, kuna sehemu nchini ambazo usalama umeathirika kwa hali mbaya. Alitaja sehemu kama Narok, Embu, Mandera, Marsabit, Tana River na kadhalika, lakini kuna sehemu nyingi zaidi kuliko hizo alizotaja. Rais alitoa wito kwamba kuwe na amani na kuwa sio vizuri kwa watu kupigana. Alisema kuwa ni lazima kila mtu awajibike katika kudumisha usalama wa nchi yetu. Vile vilie alingazia historia ya nchi ya Kenya na hatari zilizopo kwa kutokuungana. Rais alitaja Katiba katika kipengele cha Kumi ambacho kinatoa wito wa umoja wa taifa. Rais alitaja wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2007/2008 kulipokua na utovu wa usalama, ambapo watu 1,300 walipoteza uhai wao ilhali 650,000 wengine waliathirika kwa kukosa makao. Hilo halikuwa jambo jema kabisa. Lakini kwa hayo yote, Rais aliwaomba wananchi wa Kenya msamaha kwa niaba ya Serikali zote zilizokuwepo, tangu Uhuru mpaka sasa. Ndio maana mimi husema kwamba wakati mwingine, viongozi huingiwa na roho mtakatifu. Nafikiri siku hiyo, Rais aliingiwa na roho mtakatifu ndipo akatuomba wananchi wa Kenya radhi kwa maovu yote yaliyotekelezwa na kutendwa na Serikali na viongozi waliopita, kuanzia Serikali ya babake, Mzee Jomo Kenyatta; Serikali ya Moi na Serikali ya Kibaki. Sijui kama wale marais aliowaombea msamaha ambao bado wanaishi watajitapa na kusema kwamba “Kijana alifanya vizuri kutuombea msamaha” ama watanyamaza tu kama ilivyo kawaida. Lakini hivyo ndivyo Rais tuliye naye wakati huu alivyo. Bw. Naibu Spika, mwishoni, Rais alitaja mambo yanayoendelea wakati huu, hasa mambo ya ufisadi; aliyakemea na kutuambia kwamba yuko na ripoti iliyopendekezwa kwake na Tume ya Kupambana na Ufisadi ( Ethics and Anti-Corruption Commission(EACC) . Alituambia kwamba yuatupa ripoti hiyo sisi Wabunge ili tuisome vile ilivyopendekezwa kwake, tutafakari na tuamue vile tutakavyofanya. Wabunge wengine walisema “O, sio vizuri kwake kupewa ripoti kama hii;” lakini sio kosa lake! Sheria inasema kwamba EACC yafaa itoe ripoti mbili; moja iende kwa Rasi na nyingine ije Bunge. Kwa hivyo, Rais alipokea ripoti hii na akaileta hapa Bunge kupitia kwa Hotuba yake na akaifanya iwe kibandikizo cha Hotuba yake. Je, kosa alilofanya ni lipi? Alipoona imekuwa uzito kusoma ripoti hii, akaipendekeza kwa Bunge la wenye hekima ili kuyatafakari yaliyomo. Bw. Naibu Spika, nimeisoma ripoti hii; ni aibu iliyoje kuona kwamba wale viongozi walioheshimika katika Kenya hii wametajwa hapa kwa kuiba pesa za umma? Ni aibu iliyoje kwamba hata Gavana wangu wa Migori anatuhumiwa kuiba Kshs600 million kutoka katika kaunti ambayo ni masikini? Sijui nicheke au nilie; nalaani kitendo hicho kama Seneta wa Migori. Kwa bahati mbaya, kuna watu wengine katika Seneti yetu waliotajwa katika ripoti hii, Sen. Orengo akiwa mmoja wao. Tumeona kuwa amefanyiwa unyama kwa kudai haki ya marehemu babake. Ripoti hii yasema kwamba kuna Seneta mwingine mwenzetu aliyenyakua zaidi ya Kshs1 bilioni. Nadokezewa kwamba ikiwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}