GET /api/v0.1/hansard/entries/532639/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532639,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532639/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Yaliyomo kwa ripoti hii yamedokezewa kwetu na Rais mwenyewe, tuyasome, tuyaelewe na tuyachunguze. Ethics and Anti-CorrruptionCommission wamesema watayachunguza. Wamepewa muda wa siku sitini kufanya vile, lakini hizo ni chache; lakini huo muda ndio waliopewa. Wako na wafanyikazi wa kutosha na tunatarajia watupe ripoti kamili kwa muda wa siku sitini. Hiyo ni amri ya Rais wa nchi hii. Kwa ufupi, sioni makosa Rais alifanya kwa kutupa ripoti hii; ilikuwa ni wajibu wake atuambie yaliyo kichwani mwake na yale mazito aliyokuwa nayo akatudokezea sisi tuyafikirie ndiposa akatupa ripoti hii tumsaidie kimawazo. Kweli, kuna mengine ambayo hayastahili kabisa kulingana na vile yalivyoandikwa, lakini uchunguzi uendelee, ufanywe kwa undani na tuambiwe ukweli. Ni jambo la kusikitisha, kushangaza na kustaajabisha kwamba mambo kama haya yanaendelea nchini; kwamba watu wanajirundikia mamillioni ya pesa. Waziri mmoja, kwa shamba moja pale pwani, anajitakia Kshs65 milioni kama rushwa na mwenye shamba apewe Kshs 48 milioni. Hayo ni maajabu. Huo ndio kweli unaendelea Kenya. Wale Magavana ambao wamekataa kung’atuka kazini basi wapelekwe kortini; wakishafikishwa huko basi watang’atuka wenyewe. Naunga mkono ripoti hii kwa dhati."
}