GET /api/v0.1/hansard/entries/532641/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532641,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532641/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mositet",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 608,
        "legal_name": "Peter Korinko Mositet",
        "slug": "peter-korinko-mositet"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa ruhusa niweze kuchangia Hotuba ya Rais aliyoitoa kwa Bunge wiki iliyopita. Rais aliwajibika kikatiba na akazungumzia taifa lote kutoka Bunge. Aliyazungumzia mambo ambayo Serikali yake imefanya na yale ambayo yatafanywa. Rais alichangia na kusema kuwa Wizara, kama ni ile ya barabara, yale ambayo serikali ishafanya na kweli tushaona yamefanyika na yale ambayo itafanya kama mradi wa Lamu Port-Southern Sudan-Ethiopia Transport (LAPSSET) ambao utafungua upande ule mwingine wa nchi. Pia, alisema kuwa uchumi wa kitaifa umepanuka, na ni kweli. Hata kule chini, tangu pesa za ugatuzi kuanza kwenda kule kwa kila kaunti, wananchi wanahisi pesa zile ambazo zimeenda kule mashinani. Bw. Naibu Spika, Katiba yetu inatambua kwamba kuna Seneti na Bunge la kitaifa na wale waliochaguliwa ni watu walio na hekima, hivyo basi wakichangia, watachangia kwa hekima kweli kweli. Rais wetu alitueleza yale yote ambayo Serikali imefanya, ambayo ni ya ukweli kabisa. Tumeona kuwa shule nyingi zimepata nguvu za umeme; ni chache tu ambazo hazijapata huduma hii. Hasa katika kaunti yangu ya Kajiado, shule nyingi za msingi zinajivunia huduma ya nguvu za umeme. Ingekuwa pia vizuri iwapo Serikali itajaribu kuhakikisha kuwa mabwawa ya maji yaliyoko karibu na shule ama yale ambayo wananchi pia wanatumia, nguvu za umeme pia zifikishwe pale ili tuwasaidie watu wetu wanapoteka maji. Pia, tuliona ile kazi ambayo Wizara kama ya Barabara na Uchukuzi inafanya katika Jomo Kenyatta International Airport (JKIA). Lakini ni vizuri wakati mwengine pia Wizara ziwe na mikakati ya kukabiliana na janga kama lile la moto lililofika pale Jomo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}