GET /api/v0.1/hansard/entries/532643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532643,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532643/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kenya International Airport. Tunafurahia kazi nzuari ambayo inaendelea pale na ujenzi mzuri na wa kisasa ambao unatupa sura nzuri kama Kenya na tunaweza kujivunia mradi huu utakapokamilika. Ni vizuri wale wanaopewa jukumu la kufanya kazi wawe na mipango mizuri ili tuwe tayari kukabiliana na janga lolote. Rais pia alizungumza kuhusu changamoto ambazo tunazopitia. Watu wanajaribu kujitenga kikabila. Alisema hakuna kitu kizuri kama sisi kuwa kama jamii moja. Itakuwa vizuri, kama viongozi, watachangia na kusaidia taifa hili liwe na umoja. Kwa hekima na kunyenyekea, Rais aliomba msamaha kwa niaba ya Serikali za awali kwa makosa ambayo ziliwatendea Wakenya. Hilo lilikuwa jambo la busara sana. Rais alijishusha chini ili aombe msamaha. Ningependa kumpongeza Rais. Kama Wanakenya, tunafaa kujivunia Rais wetu. Yeye aliomba msamaha na hatufai kufanya mambo ambayo yatachangia kuharibu njia ambayo baba taifa ametuonyesha. Nimesikia wengine wakisema kwamba watu wanafaa kuanza kupewa haki zao. Lakini, kule kuomba msamaha ni haki kubwa sana. Rais pia alisema kuna kiasi fulani cha pesa kitatengwa kama fidia kwa waathiriwa. Hiyo ni sawa. Mambo mengine aliyozungumzia yanahusu Katiba. Kama kuna watu ambao walikosewa na ambao ardhi yao ilichukuliwa kwa njia ambayo haifai, tuna Katiba ambayo inatuongoza kuyarekebisha. Kuna National Land Commission (NLC) ambayo pia inaweza kufuatilia mambo kama hayo. Nina hakika pia, kama mmoja wa jamii ya Kimaasai, wakati utafika ambapo tutapewa haki zetu. Ardhi kubwa katika Kenya hii ilikuwa ya Wamaasai. Hata Nairobi, mahali tulipo, palikuwa pao. Mbuga ya wanyama ya Nairobi inasimama katika ardhi ambayo ilikuwa ya Wamaasai. Tunajua wanyama wote ambao wanatoka Kajiado huenda hapo. Kwa hivyo, itafika mahali ambapo tutapewa ardhi hiyo. Ilikuwa jambo la kujivunia tuliposikia Rais akiomba msamaha. Itakuwa vizuri kama Serikali itawapa chakula wale ambao wameathiriwa na njaa kama vile jamii ya wafugaji. Wakati huu ni mgumu sana kwao. Hata wakati tunapoongea mambo ya maendeleo, kuna watu ambao wana shida za vyakula. Ng’ombe, punda, ngamia na mifugo wengine wanaona shida sana. Naomba Serikali ya taifa pamoja na serikali zote za kaunti kuangalia na kuhakikisha kwamba watu hawaumii vile wanavyoumia sasa. Ikiwezekana, pesa zinafaa kutolewa ili watu na mifugo wao wasife kwa sababu ya njaa. Wakati huu, kuna sehemu ambazo zimekumbwa na baa la njaa kabisa. Kwa mfano, tuna pande za Mosiro, Mashuru na Meto. Ningependa kumuuliza Gavana wa Kaunti ya Kajiado ashughulikie mifugo na watu ili wasiumie. Ningependa pia kuuliza Mnistry of Water, Environment and Natural Resources na"
}