GET /api/v0.1/hansard/entries/532647/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532647,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532647/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Rais alimalizia kwa kusema kwamba ana hofu kwamba baadhi ya watu ambao wamepewa nafasi ili kuwahudumia wananchi wa taifa hili wamegeuka kuwa waporaji. Tume ya Ethics and Anti-Corruption Commision (EACC) ilimkabidhi Rais ripoti ambayo Rais pia alitukabidhi. Wiki moja iliyopita, Kamati ya Bunge ya Finance, Commerce and Budget ilikuwa Naivasha. Tulialika tume ambazo zinahusika na pesa ambazo zinatumwa kwenye kaunti. Tuonelea kwamba Tume ya EACC na pia kitengo cha CID wanafaa kuja hapa kufanya uchunguzi. Lakini hatukupata watu kutoka vitengo hivyo viwili. Baada ya Hotuba ya Rais, tuliona orodha ambayo Rais alitoa. Jambo la kushangaza ni kwamba Tume hiyo imejaribu kufanya uchunguzi kuhusu watu fulani lakini imeshindwa. Hii inaonyesha kuwa Tume hiyo imeshindwa kufanya kazi yake. Tume hiyo ina watu hoi hae na hawana nguvu ya kufanya vile walivyoapa kuwafanyia wananchi wa Wakenya. Ripoti hiyo ina majina ya Maseneta, Wabunge, Magavana wengi na pia wafanyikazi wengi wa Serikali. Lazima tujiulize kwa nini watu hawa tu waliwekwa katika orodha hiyo? Ingawa Tume hiyo ina dosari hapa na pale lakini watu waliotajwa lazima waajibike. Waswahili walisema; palipo moshi hapakosi moto. Wale ambao wametajwa wanafaa kung’atuka nafasi zao ili wachunguzwe. na kuzipa nafasi tume ambazo zinafaa kuwachunguza. Wananchi wanafaa kuona kwamba sheria inafuatwa. Tusiwe tukimfuata mwananchi wa kawaida anapoiba kuku au kunywa chang’aa na kumfunga kwa miaka kumi. Watu wa kawaida hufuatwa na kufungwa kwa miaka mitano au zaidi. Lakini wale ambao wamepora pesa ambazo zinafaa kuwahudumia wananchi hushinda kortini kwa miaka mingi. Hata baada ya kwenda kortini kwa miaka mingi, watu hawa huaga dunia kabla ya kesi zao kukamilika. Tunavyosema hivyo, tunajua kwamba kesi za Goldenberg na Anglo Leasing bado ziko kortini. Waliohusika mbeleni pengine wamemaliza wakati wao katika dunia hii. Ni lazima pesa za wananchi ziwafikie na kuwapa huduma. Rais alifanya jambo la busara kabisa. Rais alitupatia fursa ili kuchangia Ripoti hii kwa sababu alijua kwamba katika Bunge hili tuko na hekima ya kuweza kuangalia jambo hili. Ninaunga mkono Hotuba ya Rais."
}