GET /api/v0.1/hansard/entries/532704/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532704,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532704/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ni njia moja ya mhe. Rais kuwazungumzia wananchi pamoja na viongozi. Mhe. Rais alizungumzia mambo ya maendeleo, kwa mfano, kusambazwa kwa umeme katika mashule, pesa ambazo Serikali ya Jubilee imetenga kwa vijana, akina mama na walemavu. Bw. Spika wa Muda, mhe. Rais aliomba msamaha kwa niaba ya Serikali za hapo awali kwa makosa yote yaliyotendewa wananchi. Ningenda kuchukua nafasi hii kuwaambia viongozi wenzangu kwamba hakuna neno kubwa zaidi ya msamaha. Viongozi wenzangu wanaosema wangemtaka mhe. Rais achukue hatua nyingine ya kutatua makosa mengine yaliyofanyika hapo mbeleni, kwamba sioni kama kuna jambo kubwa zaidi ya kuomba msamaha. Ninamuunga mkono kwa kuomba msahama kwa niaba ya Serikali za hapo awali. Bw. Spika wa Muda, wakati huu wa Muungano wa Jubilee, unaoongozwa na mhe. Rais na mhe. Naibu Rais wetu, utekelezi wa maendeleo ni jambo la maana sana. Kwa mfano, utekelezi wa usambazaji wa stima kuhakikisha kwamba imefika katika kila shule ilikuwa ni jambo la ajabu kwetu. Mhe. Rais mwenyewe hajaketi; amehakikisha kwamba stima imefika katika kila shule. Pia mhe. Rais amehakikisha kwamba usambazaji wa stima umeboreshwa. Haya yote ni mambo yanayomhusu mwananchi pale chini. Haya yametajwa katika manifesto yetu ya Jubilee, kwamba lazima mambo ya maendeleo yaangaliwe kwa umakini. Bw. Spika wa Muda, mambo ya ugatuzi imejikita sana katika Katiba yetu. Tulipitisha mambo ya ugatuzi kwa sababu tulitaka maendeleo yamfikie mwananchi. Ninaposimama hapa, pesa zinazopeanwa na Serikali kuu kwenda kule chini katika serikali za kaunti zinafaa zitumike vizuri. Kwa hivyo, nataka kuunga mkono hatua yake ya kupigana na ufisadi. Hata hivyo, ukiangalia ile orodha ya watu wafisadi iliyopeanwa kwa makini, utaona uchunguzi kamili haukufanyika. Ninapendekeza kuwa kabla ya orodha kuwasilishwa kwa mhe. Rais uchunguzi zaidi ufanywe ili isiwe ni aibu kwa taifa. Bw. Spika wa Muda, ninachukua nafasi hii kuhimisha tume ya EACC kufanya kazi yake kikamilifu ya kupigana na jinamizi ya ufisadi. Inatakikana tuwe na majina yaliyofanyiwa uchunguzi kamili. Kama kiongozi, siungi mkono mambo ya ufisadi. Pesa zilizopeanwa katika kaunti mbalimbali lazima zitumike kwa minajili ya kuwanufaisha wananchi. Manifesto yetu ya Jubilee inatilia mkazo uwazi katika mambo ya pesa za wananchi. Pesa zinazopeanwa katika kaunti ama pesa zote zinazosimamiwa na kiongozi yeyote katika nchi hii yetu ya Kenya ni pesa za wananchi. Kwa hivyo, ni lazima pesa hizi zitumike kwa uwazi ili kuboresha maisha ya wananchi wote. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hotuba ya mhe. Rais. Ninawaomba wenzangu Maseneta kuunga mkono Hotuba hii. Tumunge mkono mhe. Rais kwa vyo vyote vile. Kwa hayo machache, Bw. Spika wa Muda, naunga mkono."
}