GET /api/v0.1/hansard/entries/532722/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532722,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532722/?format=api",
    "text_counter": 190,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kuna pesa ambazo hupewa walemavu ambao wana ulemavu wa hali ya juu. Pesa hizi zimekuwa zikitusaidia sana. Naomba mhe. Rais aweke kanuni za kufuata ili pesa hizo ziwafikie wanaolengwa bila shida yoyote. Ufisadi umeshika mizizi katika nchi yetu. Tunaofia kwamba pesa hizi zaweza kuwa haziwafikii wale ambao wanahusika. Tuna ripoti iliyo mbele ya Seneti ambayo ni orodha iliyotoka kwa tume ya EACC. Kwa kawaida, mtu anapotajwa katika ripoti kama hii, ikiwa anafanya kazi katika Serikali, anafaa kujiuzulu. Inakuwa vigumu kwa wale ambao wamechaguliwa kukaa kando ili uchunguzi ufanywe kutokana na sheria za Bunge. Mhe. Rais hakufanya makosa yoyote alipowauliza watu wasimame kando ili uchunguzi ufanywe. Uchunguzi haukuanza siku ambayo Mhe. Rais alipotoa Hotuba. Uchunguzi ulikuwa umeanza hapo mbeleni. Mhe. Rais alikuwa akiwaomba wale ambao wanafanya uchunguzi kuharakisha na akawapa siku 60. Tume ya EACC haifai kukaa na Ripoti ya mambo ambayo wanachunguza. Kesi zingine zimechunguzwa zaidi ya miaka mitano. Hii ni kupoteza pesa za Wakenya. Naunga mhe. Rais mkono. Siku hizo 60 zikiisha, kama mtu hajapatikana kuwa mfisadi, basi anafaa kuondolewa lawama. Wale ambao watapatikana kujihusisha na ufisadi wanafaa kustakiwa. Watu ambao wametajwa katika Ripoti ya ufisadi si wote ambao waliohusika na mambo hayo. Bila uchunguzi kufanywa, itakuwa vigumu kujua ni nani amehusika na ufisadi na wale ambao hawajahusika. Bw. Spika wa Muda, nawaomba watu wa magazeti waache kuongezea chumvi katika ripoti ambayo wanatupa. Ripoti ambayo wametupa ni tofauti sana na Ripoti hii. Watawapotosha Wakenya ili wasielewe kinachoendelea. Nawaomba waandike mambo kwa magazeti wakizingatia ukweli badala ya kuweka maneno matamu ili magazeti yanunuliwe. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hotuba ya mhe. Rais na Ripoti ya EACC."
}