GET /api/v0.1/hansard/entries/532728/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532728,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532728/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ninampongeza mhe. Rais kwa hatua ya kusema kwamba Kshs10 bilioni zitatengwa kwa kuwafadhili wale ambao waliathirika katika maisha ya hapo awali. Kwa mfano, kuna Wabajuni ambao walikuwa wakikaa sehemu ya Kiunga ambao wamepoteza miji yao, mali yao na nafsi zao na wakakimbilia Lamu, Kilifi na Malindi. Hao ni watu ambao walitoka Kiunga, Ishakani na Rubu. Miji hiyo ilivunjika wakati ule ambao kulikuwa na vita vya Shifta. Isisahaulike ya kwamba, mwaka uliopita watu wetu kule Mpeketoni walipoteza mali yao na hata maisha yao. Kwa hivyo, inafaa wasisahaulike wakati pesa hizo zitakuwa zinagawanywa. Ningependa kupongeza Serikali ya Jubilee kwa kupiga hatua kubwa kwa kusambaza umeme kila mahali, hasa kwa shule nyingi hapa nchini. Huu ndio msingi wa kuweza kuleta and kuzitumia zile tarakilishi za watoto wa shule. Vile vile viongozi wengine husema kwamba kupanda kwa thamani ya Shilingi ya Kenya kwa dola inamaanisha nguvu ya uchumi wa nchi ya Kenya. Hii inarahisisha ulipaji deni katika benki. Hii inalingana na thamani tofauti ya sarafu za ulimwengu. Tulifurahi mhe. Rais aliposema kwamba kwa wiki mbili zijazo, miradi kadhaa wa kadha itatekelezwa na yeye mwenyewe atatembelea mji wa Lamu ili kuanzisha ujenzi wa Bandari ya Lamu na vile vile ule mradi wa LAPSSET kuanzia Lamu hadi sehemu zingine za Kenya. Huu mradi utakuza biashara na kuleta utajiri mwingi katika nchi yetu. Inafaa tumuunge mkono mhe. Rais Uhuru Kenyatta kwa huu mradi. Ninawashukuru wale Maseneta wengine ambao wameunga mkono Hotuba hii."
}