GET /api/v0.1/hansard/entries/532741/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532741,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532741/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ulipopatikana katika Pwani ya Kenya, watu waliathiriwa sana, hasa katika ufisadi wa mashamba. Pwani yote kwa ujumla ni kama maskwota. Hivi sasa, mhe. Rais aliomba msamaha na kusema kwamba kwa niaba ya watu walioongoza taifa letu la Kenya hapo awali; Mzee Kenyatta na Kibaki wasamehewe kwa makosa yao. Sisi tunasema kama watu wa Pwani, wakitaka tuwasamehe sisi na tukubaliane nao, basi hizo hati za ardhi zote walizopewa kiholela zirejeshwe ndio tutasema ni sawa kwa msamaha. Lakini kama hazijarudi, hatuwezi kukubaliana na huo msamaha. Kuhusu usalama wa nchi, usalama katika Mkoa wa Pwani umekuwa wa hali ya taharuki. Hakuna usalama unaowekwa na polisi. Hakuna usalama unaowekwa na kipengele chochote na wafanyakazi wa Serikali. Tunachoona ni dhuluma tu kila siku."
}