GET /api/v0.1/hansard/entries/532746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532746,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532746/?format=api",
"text_counter": 214,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Waswahili husema, “Mwanzo wa ngoma ni lele.” Sisi kama Wakenya tunaona tuna mwanzo mwema hapa. Ukiangalia ndani ya Seneti hii utaona kuna matumaini na hamu ya kuona Kenya inapoelekea. Bw. Spika wa Muda, wangapi kati yetu wanaomba msamaha? Mhe. Rais ametoa mfano mwema hata mpaka kwa watoto wetu na vizazi vyetu. Nimesimama hapa kama mama ambaye amejifungua na ukiangalia huduma hospitalini, ni kitu cha kufurahisha sana. Kitu ambacho ninaomba tukitilie mkazo ni kuangalia pia kabla ya kuzaa. Akisha jifungua mama tutafanya aje ili nchi yetu ielekee na kujua kwamba mwanamke amezalishwa bure. Kwa hivyo, tutafanya aje kabla na baada ya kuzaa? Hii ni zawadi mwafaka kwa hii Sikuu ya Pasaka. Unapotembea njiani, utajua kwamba Kenya kuna mabadiliko. Bw. Spika wa Muda, tukiungana sote kama Wakenya ama kama Maseneta, nchi yetu itaenda mbele. Kila mtu ambaye amekula chakuka kisichofaa ama kila mtu ambaye amekula hongo arudishe kwa sababu hicho chakula sio chake. Lazima chakula chochote kiwe ni halali unapokitumia."
}