GET /api/v0.1/hansard/entries/532747/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 532747,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532747/?format=api",
    "text_counter": 215,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 758,
        "legal_name": "Boy Juma Boy",
        "slug": "boy-juma-boy"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ya kusema machache juu ya Hotuba ya mhe. Rais. Kwanza, namsifu aliyeandika Hotuba hii. Hotuba hii iliandikwa kwa umarufu sana. Pili, ninamsifu mhe. Rais kwa kuisoma Hotuba yake kwa ufasaha wa juu. Tatu ni swali: Je, ndio mara ya kwanza Hotuba nzuri kama hii kusomwa hapa Bungeni? La. Marais wengine wameshatoa hotuba nzuri kama iliyosomwa na mhe. Rais Uhuru. Je, kuna matokeo baada ya hotuba? Hilo ndilo jambo muhimu sana. Bw. Spika wa Muda, kwa mfano, tuliambiwa kutakuwa na elimu ya bure. Kweli kuna elimu ya bure hapa nchini? Leo hii, elimu ya shule za msingi ni ya bure? Tunaambiwa kutakuwa na elimu ya bure ya sekondari. Hiyo ni porojo tu. Tukiingia katika suala la kuomba msamaha kwa Wakenya, namsifu sana mhe. Rais kwa kuomba msamaha. Je, ni nini anachoomba kusamehewa? Huo msamaha waombwa wa jambo gani? Ni lazima tuelewe msamaha unaombwa kwa sababu ya jambo gani. Msamaha aliouomba haueleweki. Bw. Spika wa Muda, tukiingia kwenye swala la ufisadi, huu ni mchezo . Ninawasihi wafuasi wa CORD wasiingie katika mchezo huu. Hii ni kwa sababu hapa tumeshapigwa mbao moja kwa sufuri. Huu ni mchezo na siku moja sisi tutakuwa ndani kama CORD na wao watakuwa nje. Waingereza husema hii ni: Game plan."
}