GET /api/v0.1/hansard/entries/532785/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532785,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532785/?format=api",
"text_counter": 25,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Ninakushukuru, Bw. Naibu Spika. Nimefanya kazi na Rais Uhuru Kenyatta nikiwa Kiranja wa Serikali katika Bunge naye akiwa Waziri wa Fedha. Nilimtumikia Waziri wangu katika Bunge la Kumi kwa uaminifu. Yeye anaweza kutoa ushahidi hapa kusema kwamba kamwe hakuna siku ambayo nilikanyaga katika ofisi yake kumuomba usaidizi wowote. Pia niliwatumikia Sen. Murungi na Sen. Haji ambao wako hapa. Ninasema haya kwa sababu, ili tutoe shida katika nchi hii, inafaa tumalize magendo, rushwa na hongo. Kutenda jambo hili ni kazi ngumu na lina uzito mkubwa sana kwa sababu ni lazima uanzie mahali fulani na watu fulani. Maneno ambayo mhe. Rais Kenyatta aliyasema akitoa hii Ripoti, alithibitishia nchi kwamba katika Ripoti hii kulikuwa na majina ya watu fulani ambao walihofiwa kuhusika kwa ufisadi na angependa Bunge itoe mwelekeo. Tangu tupate Uhuru, kumekuwa na wizi wa mali ya umma. Lakini kila mtu aliyeitumikia Serikali; awe mwanasiasa ama mtumishi wa Serikali, wote wamekuwa makasisi na masheikh; hakuna anayeweza kukubali ya kwamba anafaa kuchunguzwa na kushtakiwa. Kwa hivyo, ninaanza kuchangia Ripoti hii kwa kusema kwamba, ili totoe mambo haya. Ni lazima kuwe na chanzo cha kila jambo. Hapa, chanzo chake ni binadamu ambao ni Wakenya. Kati ya wale wahusika, kuna wale wenye hatia na wale ambao hawana hatia. Swali ni: Je, tutakubali lini kwamba kuna watu ambao wana hatia na wengine hawana hatia? Bw. Naibu Spika, hata kama niko katika ripoti hii, ningependa kusema ya kwamba, kwa mara ya kwanza, Rais Uhuru Kenyatta, ameonyesha ujasiri mkubwa sana kwa kutamka na kupeana orodha kama hii. Alifanya hivyo bila kujali angebaki na nani katika Serikali yake. Yeye hakujali nani atayemuabudu, atayemkashifu na atayewezakukaa vipi katika madaraka. Wakati wa Rais Msitaafu Kibaki, kulikuwa na Mawaziri ambao Bunge letu liliwahitaji kuondoka ni mamlakani ili wachunguzwe. Hata hivyo, mhe. Rais Kibaki hakusema lolote kuwahusu Mawaziri hao. Rais Msitaafu Moi pia alikuwa na Mawaziri wake ambao tunakumbuka sarakasi zao. Wakati Mhe. Robert Ouko alipouwao, Rais Moi wakati huo alitangaza kwamba washukiwa wote washikwe na kutiwa mbaroni. Waziri kama vile mhe. Biwott alishikwa lakini akapitia mlango wa nyuma na kuwa huru. Bw. Naibu Spika, Rais Uhuru wakati walipotoa hotuba hapa alisimama na kusema mtu yeyote ambaye ametajwa katika ripoti hii; awe Gavana, Waziri, Seneta, Katibu Mkuu na wengine wote, wang’atuke mamlakani. Lakini, Maseneta hawana ofisi za kuzuia uchunguzi kufanywa. Wanaotakiwa kuondoka ni wale ambao wametumia mamlaka yao Serikalini kujinufaisha wenyewe. Sisi kama Seneti na Wakenya wote kwa jumla, tungependa wote waliotajwa kwenda nyumbani ili wachunguzwe na tume husika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}