GET /api/v0.1/hansard/entries/532787/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532787,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532787/?format=api",
"text_counter": 27,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mimi nimetajwa hapa kwa sakata ya shamba la Malili. Ndugu na dada zangu, ukitazama ukurasa wa tatu katika ripoti hii, jina langu ni nambari saba. Hata hivyo, hatujui ni pesa ngapi zinahusika hapa. Mimi nilipelekwa kortini, nikasimama kizimbani na kutoka baada ya kulipa bondi ya Kshs1.5 milioni. Kwa hivyo, ni korti ndio itaamua ni nani mwenye kusema ukweli na uongo. Bw. Naibu Spika, ili tuandamane na kusafisha taifa letu, tukubali mambo haya. Kilicholeta sarakasi kubwa, ni wale waliompa Rais ripoti hii. Mimi namuomba Rais, kwa ujasiri huo, awaite walioiandika ripoti hii. Ripoti hii ni aibu kubwa kwa taifa letu. Anafaa aamuru wote wakamatwe na kuwekwa ndani. Nimetajwa tena katika ukurasa wa 23 nikihusishwa tena na shamba la Malili. Mimi niliitwa na maafisa wa idara ya upelelezi ya CID na nikaenda. Waliniuliza maswali na nikawajibu. Walisema nilikuwa na kesi na nikapelekwa kortini. Sasa hapa tena, yanarudia makosa yale yale. Kwa hivyo, hawa watu wamefanya kazi duni kwa kumpatia mhe. Rais ripoti hii. Mhe. Rais ana nia ya kufanya kazi safi lakini kizingiti ni maneno haya yalioandikwa hapa ambayo hayafai. Bw. Naibu Spika, ukitazama ukurasa wa 45---"
}