GET /api/v0.1/hansard/entries/532789/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532789,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532789/?format=api",
"text_counter": 29,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, page ni ukurasa. Sura ni chapter. Nimetajwa kwamba nafaa kuchuguzwa kwa ujenzi wa barabara iliyogharimu Kshs57milioni. Pesa nilizopokea za juu zaidi zilikuwa Kshs8 milioni. Tuliofanya kazi pamoja na Sen. Haji. Ndio mradi kama huo upite, ilikuwa ni lazima bodi ya ConstituencyDevelopment Fund (CDF) ikae chini na kuupitisha. Hakuna mradi ambao ungegharimu Kshs57milioni. Kasheshe na msukosuko ni kwamba, Waziri wa Kilimo anachunguzwa kwa jambo moja. Bw. Waziri kwa kuwasaidia Wakenya na kuwaonyesha kwamba kilimo kina maana anashtakiwa kwa kukodisha sehemu ya shamba ya Serikali. Waziri huyo hajaiba au kunyakuwa shamba hilo. Inasemekana hapa kwamba ameikodisha na kulima ekari 100 na kuwaajiri Wakenya pale kufanya kazi. Kama Waziri wa Kilimo, anawaonyesha Wakenya jinsi ya kutia bidii katika ukulima, je, huo ni ufisaidi? Hivi sasa, ameachishwa kazi na anachunguzwa kwa jambo hilo. Hayo ndio mambo yalioko hapo. Nataka kumwambia mhe. Rais kwamba Wakenya walishangaa walipomuona akitabasamu wakati alipokuwa akiwakabithi Maspika Ripoti hii."
}