GET /api/v0.1/hansard/entries/532797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 532797,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/532797/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nashukuru kwa kufahamishwa na Sen. Sang. Ni kweli na dhahiri kwamba Waziri anakashifiwa kwa kumuweka msaidizi wake kusimamia shamba ile. Sisi tunawatafutia Wakenya kazi bila kujali kabila lao. Lakini la kuhuzunisha ni kwamba, Waziri wa Kilimo anapigwa kumbo kwa mambo hayo. Bw. Naibu Spika, nimesoma madai kuhusu Waziri Kamau. Mimi simtetei, lakini nimefanya kazi naye, akiwa Katibu wa Kudumu katika Serikali iliyopita. Mimi nimemtembelea ofisini zaidi ya mara 50. Chochote nilichomuuliza yeye kufanya, alikizungumzia kwa kina akieleza barabara atakazo shughulikia, zile hangeweza shughulikia kutokana na ukosefu wa pesa na zile angeweza kuzitafutia pesa. Hakuniitisha hongo hata siku moja. Inakuwaje kwamba Waziri Kamau yuko mashakani kwa kupeana kandarasi ya mradi wa reli uliotangazwa katika nchi hii kila siku na hata Rais mwenyewe akauwazisha rasmi? Kwa nini Rais mwenyewe alienda kufungua ule mradi kama kandarasi ilikuwa na shaka? Je, tuko na Serikali ambayo inafanyia Wakenya kazi ama ni kufanya kazi ya kucheza mpira wa miguu? Ni aibu sana kwa sababu Eng. Kamau yuko nyumbani kwa sababu ya huu mradi na ilhali kazi inaendelea. Mhe. Rais anausifu mradi na ilhali Eng. Kamau anakula maharagwe nyumbani. Nani mwenye haki? Ni lazima tukubaliane. Mimi ninasema kwamba mhe. Rais aliingia Bungeni na Wakenya walikuwa na matarajio makubwa. Mhe. Rais alizungumza maneno mazuri sana lakini tabasamu yake iligeuka kuwa kilio. Baada ya kutoa Ripoti hii, kila mtu alipiga makofi. Mimi niliona mhe. Wetangula na mhe. Orengo wakiwa wa kwanza kusimama kupiga makofi kumsifu na kumshangilia mhe. Rais kumbe walikuwa wanashangalia Ripoti duni. Sasa kicheko hicho kimekuwa kilio. Kwa hivyo, mimi nauliza kila mtu aliyetajwa hapa achunguzwe na kila mtu ajisafishe na aende nyumbani. Wale watakaopatikana na hatia, waende nyumbani na kufungulia mashtaka. Bw. Naibu Spika, kuna wezi ambao hawakutajwa katika Ripoti hii ingawa ni wezi sugu. Mimi husimama mkutanoni na kusema kwamba Serikali ya Jubilee ina wezi wengi lakini sijawahi kufafanua zaidi. Leo nataka kutangaza kwamba mhe. Uhuru Kenyatta hajui kuiba. Lakini wanaomzunguka, ni wezi hatari. Ni bahati kuwa anaenda nyumbani akiwa amevaa viatu vyote viwili. Wale ni wezi sugu sana; wana ujuzi wa wizi."
}