GET /api/v0.1/hansard/entries/533018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 533018,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/533018/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Madam Spika wa Muda, sisi kama viongozi, ni lazima tuige mfano uliotolewa na Rais wetu, Uhuru Kenyatta. Hatua hii ya Rais ni ya kusisimua na kupendeza; yafaa kuigwa na watu wote. Sisi, kama viongozi, ni lazima tuzungumze ukweli na tufuate mwenendo mzuri kama huu. Madam Spika wa Muda, kuambatana na habari iliyotolewa hapa na Rais kuhusu ripoti ya Tume ya Kupambana na Ufisadi ( Ethics and Anti-Corruption Commission ) iliyowasilishwa hapa, inasema kwamba ripoti hiyo sio ya ukweli; inasema kwamba ripoti hii imetayarishwa kwa njia ya mapendeleo. Tuko na uhakika kwamba kuna ufisadi unaofanyika katika kila pembe ya Kenya hii. Ufisadi sio wa watu fulani peke yao; ufisadi umemea mizizi mpaka huko vijijini."
}