GET /api/v0.1/hansard/entries/533023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 533023,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/533023/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ukora wenyewe huanzwa hapa. Gavana, ambaye ni mkora mkuu Tana River, hakutajwa na ametajwa mtu ambaye hakuhusika. Tunataka ukweli upatikane Kenya hii kwa sababu kuna watu wanaofanya ufisadi usiweze kuchunguzwa na Auditor-General ama EACC. Ukora unaanzia hapo. Madam Spika wa Muda, ningependa kuwaomba Wakenya msamaha kwa sababu tumelala. Tumezungumza mambo mengi lakini hatujafika kule tulikokuwa tukitaka kufika kwa sababu ya wakora kama hawa wanaotuletea habari za uongo za kuwadanganya Wakenya na kuwafunga macho. Kwa hivyo, namwomba Rais Uhuru Kenyatta achukue hatua madhubuti, hata kama ni kuleta wachunguzi kutoka nchi za nje. Hatuwezi kuthamini ripoti kama hii kwa sababu haina mwelekeo au thamani yoyote. Asante, Madam Spika wa Muda."
}