GET /api/v0.1/hansard/entries/533733/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 533733,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/533733/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Asante Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii. Shukrani kwake Mheshimiwa Katoo ole Metito kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Hotuba hii ya Rais. Kwanza kabisa naanza na mambo ya usambazaji wa nguvu za umeme kwa shule za msingi. Ni jambo la busara ambalo limetupa nafasi ya shule takribani 70 katika Eneo la Uwakilishi Bunge la Magarini ambazo zitanufaika na mradi huo. Hali hiyo itaweza kusaidia wakati shule zitakapopata vipakatalishi kama ilivyoahidiwa. Nikiingia kwa upande wa ufisadi, ni wakati kila mmoja anapaswa abebe msalaba wa matendo yake. Hata hivyo, kuna sehemu zile ambazo zimenyakuliwa. Mashamba yamenyakuliwa. Ingekuwa vyema iwapo hatua zingechukuliwa kwa waliohusika na pia mashamba yale yarudishiwe wenyewe. Nazungumza hususan kuhusu mashamba ya chumvi. Kuna wale wawekezaji wa chumvi ambao walinyakua sehemu zinazomilikiwa na wenyeji. Hivi sasa wamegeuza, badala ya ukuzaji wa chumvi, wanapanda miti kinyume cha wananchi."
}