GET /api/v0.1/hansard/entries/534787/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 534787,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/534787/?format=api",
"text_counter": 328,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ya mapunzi ya kikao cha Seneti. Leo hii tuna huzuni na tunaomboleza katika nchi yetu. Wakenya wenzetu wameadhirika. Naomboleza na ndugu zangu walio huko Garissa. Kabla sijaendelea, naomba Mungu azirehemu roho za wale waliohadhirika. Tunaomba kwamba Mungu atawafariji wazazi wa Garissa ambao watoto wao walipata shida. Huu ni wakati wa Seneti kusimama wima na kukabiliana na matatizo yanayoikumba Kenya yetu. Seneti inategemewa sana na Wakenya kwa sababu huwa inasimama wima na kutetea ukweli. Tangu Seneti ianze kukaa, sijasikia Wabunge wakizungumza mambo ya mishahara. Jambo la muhimu katika maisha ya binadamu ni kupata amani. Amani haitapatikana hadi kila mmoja atakapochukua au kushughulikia majukumu yake. Mambo ya usalama wa nchi yetu hayajachukuliwa kuwa ya muhimu. Askari ambao wanatulinda ni kama wanafanya kazi ya kujitolea. Askari wa Kenya Police, Administration Police na Regular Police wanapata misharaha duni sana. Kama mishahara ya maofisa wa polisi haiwezi kuwatosheleza itawezekana kuwategemea kutulinda? Ikiwa wale ambao wanalindwa wanaiba mamilioni ya pesa kupitia kwa ufisadi, ni kwa nini huyo askari asiwe mfisadi? Mshahara wa askari wa kawaida baada ya kutoa zile mikopo alizonazo anabaki na Kshs1,800. Je, huyu askari atafanya kazi? Al Shabaab wakimpa Kshs500,000 watawapisha na hata wataingia hapa Bunge. Askari wetu wanahitaji mshahara wa kutosha ili wafanye kazi ya ulinzi vyema. Hata mimi ninaogopa wale askari wanaonilinda kwa sababu wao pia ni binadamu kama sisi ilhali wanapata mshahara mdogo na tunawahitaji kutulinda katika boma zetu. Hatutasaidika ikiwa tutategemea wanajeshi peke yao. Maafa haya yanatendeka hapa nchini na wale wanaotulinda hapa nchini ni hawa askari wa kawaida. Askari wa kawaida wanalipwa Kshs20 kwa siku kama Hardship Allowance, je watatulinda vipi? Ikiwa magavana, maseneta na wabunge wanaiba, askari wa kawaida watakoma kuiba? Kwa hivyo ufisadi na hali mbaya ya usalama vinaenda sambamba. Tutadumisha usalama hapa nchini ikiwa kila ofisa wa Serikali atapata haki yake kwa sababu hakuna mtu ambaye ni bora kuliko mwingine. Ninaunga mkono Hoja hii."
}