GET /api/v0.1/hansard/entries/534938/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 534938,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/534938/?format=api",
    "text_counter": 114,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nakara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2926,
        "legal_name": "John Lodepe Nakara",
        "slug": "john-lodepe-nakara"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika, ningependa kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hotuba ya Rais kwa Taifa. Kwanza, ningependa kumshukuru Rais kwa Hotuba yake kwa taifa ili tujue mafanikio, changamoto na mambo ya usoni katika nchi hii. Rais ametimiza ahadi ambazo alitoa katika Manifesto yake ya Jubilee. Jambo la kwanza, alituahidi kwamba atafufua uchumi wa nchi hii. Kwa kweli, uchumi wa nchi hii umefikia asilimia sita. Hiyo ni maendeleo. Aliahidi kwamba kila shule ya msingi ya umma itawekwa stima. Kati ya shule 20,500, shule 18,400 zimewekwa stima. Ingawa tunafurahia hayo, katika kaunti ninayotoka ya Turkana, watu wangu wa Mji wa Lodwar hawajapata stima kwa wiki nzima. Wafanyabiashara wamepata hasara. Wenye maduka wamepoteza vitu ambavyo vinahifadhiwa kwa kutumia stima. Hoteli zimeenda hasara kwa sababu ya kutokuwa na stima. Ingawa Rais alikuwa ameweka mkazo kwa mambo ya stima, naomba stima ya Lodwar iwe inatoka Turkwel kuliko kutumia jenereta ambayo imechangia hasara katika kaunti ya Turkana. Rais pia alitoa miradi ambayo ameibuni kwa ajili ya kuinua maisha ya Wakenya, kwa mfano, kunyunyizia mashamba maji. Ikiwa nchi hii itaelekea katika njia hiyo, hata kaunti ya Turkana, ambayo haina ardhi nzuri ya ukulima, ikipata maji na kunyunyizia kwenye mashamba, shida moja itakuwa imetatuliwa. Tutapata chakula katika udongo wetu. Rais pia aliongea juu ya ujenzi wa reli ya kisasa. Hiyo reli itabuni nafasi nyingi za kazi kwa vijana na itafanya uchumi wetu kuinuka. Tunakubaliana na Rais ya kwamba mradi wa LAPSSET pia unaweza kuchangia nafasi za kazi kwa vijana wetu katika nchi hii. Rais alichangia mambo ya ujenzi wa barabara, lakini kuna shida. Katika Kaunti ya Turkana, tumepoteza maisha ya watu wengi. Biashara kati ya Turkana na sehemu zingine za Kenya haiendi vizuri. Ukijaribu kupitia barabara kutoka Kitale hadi Lodwar, ni kama unaenda mbinguni. Barabara ni mbovu katika Kenya nzima. Hakuna barabara iliyo mbaya zaidi katika nchi ya Kenya kwa Karne hii ya 21 kama barabara ya Turkana. Tunaomba Rais aangalie mambo ya barabara za Kaunti ya Turkana. Katika sekta ya usalama, tunashukuru mahali ambapo Serikali imefanya vizuri. Lakini kila wiki katika Kaunti ya Turkana, tunazika mtu ambaye ameuliwa barabarani, ama kwa sababu ya kuchunga mbuzi wake. Hakuna wiki inapita katika Kaunti ya Turkana bila kuzika mtu aliyeuliwa. Kama vile Mheshimiwa Cheptumo alisema, tunaomba Serikali iangalie hali ya usalama ambayo imezorota kati ya Turkana, Pokot na Baringo. Watu wetu hawalali na hawana wakati wa kwenda shule kwa sababu ya hali ya usalama. Nikimalizia, tunaunga mkono msimamo wa Rais juu ya ufisadi. Watu wengine wanasema kwamba Naibu wa Rais, William Ruto, ndiye amepoteza zaidi na pengine, kabila lake halisikii vizuri. Sisi kama Wakenya tunasema msimamo wa Naibu wa Rais, William Ruto, kukubali marafiki wake na watu ambao wako karibu na yeye kuondoka afisini kwa muda ni ishara ya kwamba yeye ni kiongozi anayetaka mabadiliko katika nchi ya Kenya, hasa kwa mambo ya ufisadi. Watu wetu wanasema kwamba hao wakae kando na wafanyiwe uchunguzi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}