GET /api/v0.1/hansard/entries/535002/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 535002,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535002/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "Kwanza kabisa, ni vizuri kila mtu ambaye anaongea mbele ya Bunge hili ajue kwamba heshima inahitajika. Tukija hapa ni lazima tukumbuke kwamba Rais ambaye tunaongea kumhusu amechaguliwa na nchi nzima ya Jamhuri ya Kenya. Hatupaswi kumwambia vile anavyostahili kufanya. Kwa mfano, kusema kwamba Rais anafanya hivi kwa sababu kuna mgeni anakuja ni kumkosea heshima. Samahani kwa sababu naona Mbunge ambaye amesema hivyo ameondoka. Hatuwezi kusema kwamba katika nchi ya Kenya tutakuwa tukifanya kazi kwa sababu mtu fulani anakuja nchini. Kila mtu alifurahia mambo yaliyoendelea siku hiyo. Sisi tunasema kwamba hatuna shaka na Rais kuhusu yale aliyotuambia hapa Bungeni. Tuko na uhakika kwamba ataendelea kusaidiana na sisi katika mambo yote aliyoyasema. Nashukuru sana kwa sababu ukienda katika maeneo bunge yetu, utaona kuna kazi nyingi sana zinazoendelea. Sisi tunasema kwamba akina mama na vijana wamefurahia kubuniwa kwa Hazina ya Uwezo. Wameanza kuitumia na wanaendelea. Miradi inayowahusu akina mama imenigusa sana. Akina mama wakiingia katika chumba cha kuzalia, watazaa watoto na kupewa neti bila malipo. Siku hizi kuzaa hakulipishwi. Mimi nimewaomba wakazi wa Ruiru na waheshimiwa wenzangu watie bidii sana tuzae watoto wengi kwa sababu ni vizuri tukiwa na watoto. Mimi tayari ukiniangalia nimejitayarisha na niko karibu kwa sababu najua kuzaa kutanisaidia. Tafadhali, hayo nimesema ni yangu. Kwa sababu mimi ni mama, kujifungua ni kawaida. Naona akina mama wengine watanifuata nyuma ili katika miaka ya mbeleni, tuwe na kura nyingi. Wazee wamepata pesa kidogo za kuwasaidia maishani mwao. Tusiseme kwamba Rais anaangalia upande mmoja wa nchi kwa sababu hata sisi tukiwa hapa Bungeni, utasikia mtu akisema tunapendelea wadi moja kuliko nyingine. Hayo ni maoni ya watu. Yale ambayo mimi najua ni kwamba Rais anaangalia pembe zote za Jamuhuri ya Kenya. Simtetei lakini sio vizuri sana kusema kwamba Rais anaangalia kabila fulani. Nimesikia wengine wetu hapa wakisema Rais anaangalia Kiambu peke yake. Kuhusu vitambulisho, kila mtu anapaswa ajipange na watu wake, awasaidie kuchukua vitambulisho kwa sababu ni shughuli ambayo inaendelea. Nasema kwamba tumshike Rais wetu mkono ili sisi sote tuendelee mbele. Tumefurahi vile Rais alisema asamehewe. Mkubwa wa nchi nzima akisema: “Mnisamehe”, sisi tunajua ina maana nzito. Kama vile Mbunge mwenzangu amesema pale hadi nikafikiria anataka kuchukua kiti changu cha pasta, ni kwamba hata kama ni mtu mwenye dhambi, tunafaa kumsamehe. Kila mtu ana dhambi ya aina yake na hivyo basi, tusiseme eti tuendelee kumkanyaga Rais ili aendelee hivyo na hali amesema “pole”. Binadamu ni binadamu na anaweza kuwa na makosa. Hatujui ni nini kinachoweza kufanyika tukiwa katika huu uhai. Kwa hiyo, naunga mkono na nauliza Wabunge wenzangu tumuunge mkono Rais wetu ndio aendelee kusaidia nchi yetu. Ahsanteni."
}