GET /api/v0.1/hansard/entries/535022/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 535022,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535022/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Mimi pia ningependa kuchukua nafasi hii nimshukuru Rais kwa Hotuba yake na yale aliyotupatia wiki iliyopita. Nilifurahishwa sana na mambo; Rais alisema kwamba hatutalipa pesa za mtihani wa kidato cha nne na pia darasa la nane. Hiyo ilinifurahisha sana kwa sababu kuna watoto wengi ambao wameishi katika maisha magumu, ama wanaishi katika maisha yasiyo sawa na hawangeweza kulipa pesa za mtihani."
}