GET /api/v0.1/hansard/entries/535027/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 535027,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535027/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Kile pia ningependa Rais asisitize ni mambo ya mashamba. Kweli tumekuwa na ufisadi kuhusu mambo ya mashamba kwa sababu kuna matapeli wanaojaribu kupata vyeti, ama title deeds, vya mashamba yasiyo yao. Kama hivi juzi nilikuwa Cherangany. Kuna shule moja iliyokuwa imenyakuliwa shamba lake. Halikuwa jambo zuri kwa sababu unyakuzi wa mashamba umezidi sana katika nchi yetu ya Kenya. Ningependa Rais aorodheshe majina ya wafisadi ama watu wanaojaribu kunyakua mashamba yasiyo yao. Unaona kwamba shule nyingi hazijapata title deeds, lakini ninataka kumshukuru Rais kwa sababu amesema kwamba ifikapo mwaka 2017, title deeds milioni tatu ziwe zimetolewa kwa watu wanaostahili. Ningependa hiyo iharakishwe sana kwa sababu katika Trans Nzoia kuna mashamba kama Matunda na Cherangany. Haya mashamba hayajatolewa title deeds; kama moja ya haya mashamba litapata title deeds, tutafurahi sana."
}