GET /api/v0.1/hansard/entries/535151/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 535151,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535151/?format=api",
    "text_counter": 75,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Asante sana, mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono suala hili la kuongeza muda ili kesho tuweze kupata kikao haswa kufuatia kanuni za Bunge hili; tutatumia Kanuni ya 30(3)(b) ili tuweze kuzungumza na kuhakikisha kwamba kazi ambazo zimetuleta hapa zinamalizika kabla ya kwenda likizo. Masuala ambayo Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni ameyataja ni muhimu na itakapofika kesho jioni wakati tunaenda kusherehekea pasaka tujue kuwa tutarudi katika muda ambao umefaa; inafaa tuwe tumemaliza masuala yote ambayo yatakuwa kwenye kamati na hatua ya tatu. Tunataka tuende tukiwa katika hali ya utulivu na kuweza kuzungumza na waliotuleta kwenye Bunge hili bila wasiwasi. Asante sana mhe. Spika, na naunga mkono."
}