GET /api/v0.1/hansard/entries/535215/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 535215,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535215/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Asante sana mhe Spika kwa kunipatia fursa hii ili nami nichangie Hotuba ya Rais. Kwanza, ningependa kumpongeza Rais kwa Hotuba yake ambayo aliweza kutoa. Kulingana na Hotuba yake alizungumzia upanuzi wa bandari yetu ya Mombasa. Alisema hivi sasa inafikia kituo cha 19 na yuko katika mipangilio ya kuongeza vituo vya 20 na 21. Nikiwa Mbunge wa pale Jomvu, nasema kuwa katika kupanua bandari hiyo bila kupanua miundo msingi itakuwa ni shida kwa sababu ya msongamano mwingi. Ndani ya bandari ile ya Mombasa kutoka vituo vilipokuwa tano na sita, barabara zilikuwa ni hizo hizo. Leo mhe Rais anazungumzia vituo 19, 20 na 21 na bado barabara hazijaweza kuongezwa. Kwa maana hiyo kuna msongamano mkubwa katika sehemu za Changamwe, Mikindani, Jomvu na Miritini; shida kubwa itaweza kutupata. Rais amezungumuzia kuhusu malipo kwa wale waliodhulumiwa, lakini ni lazima pia katika fikira zangu kuangalia wale ambao wanafanya kazi na kutoa huduma katika nchi hii, na ambao hawapati fidia yoyote. Kwa hivyo, katika Kshs. 10 bilioni ambazo zilikuwa zimetengewa wale waliodhulumiwa pekee, naona pia Rais angezingatia wale The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}