GET /api/v0.1/hansard/entries/535216/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 535216,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535216/?format=api",
    "text_counter": 140,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "mabalozi wa Nyumba Kumi na pia wahudumu wa afya ambao tunawaita CommunityHealth Workers, kwa ile kazi nzuri ambayo wanafanya na hawapati malipo fulani. Kuhusu mambo ya ufisadi, nampongeza Rais kwa ile hatua ambayo amechukua kijasiri. Lakini kitu ambacho ningependa kusema ni kwamba kabla wale ambao wametajwa hawajaweza kutajwa, ilikuwa ni lazima uchunguzi kamili ufanyike. Kwa shauri tukiangalia katika hii Hotuba ya Rais na Ripoti ambayo tumepata kutoka kwa Tume ya Ufisadi--- Nikizungumzia tu kuhusu Kaunti yangu ya Mombasa, Gavana wa Kaunti yangu Ali Hassan Joho, naona ametajwa na tuhuma kuhusu soko. Soko hilo halikutajwa kuwa yeye amelinyakua, lakini limetajwa kuwa yeye alihusika katika kuondoa wahalifu ndani ya soko ambalo lilikuwa limechomeka. Baada ya soko kuvunjika, sasa soko lile limejengwa kupitia kwa watu wengine ambao ni wawekezaji wa kibinafsi. Tunaona kuwa jina lake linatajwa kando na wala hajapelekwa popote kuandikisha taarifa. Pili, katika hatua hiyo, ndugu yangu ambaye nimekaa naye hapa karibu mhe Awiti ni Mbunge wa Nyali. Ripoti ya ufisadi imemtaja kwamba amechukua kshs200 million kule Homa Bay na hali yeye yuko hapa na Homa Bay kuna wenyewe. Kwa hivyo, yule ambaye alimshauri Rais ni lazima angemshauri kisawasawa. Kuhusu mambo ya reli, tunaona kuwa Rais amesema kuwa inaendelea kutengenezwa. Lakini kitu ambacho hatukukisikia kutoka kwa Rais ni malipo kwa wale wenyeji ambao reli ile itapitia kwao; wako mabwenyenye ambao wana makaratasi na watachukua fidia zile kwa njia za kiufisadi na wenyeji watapata shida. Pia katika mambo haya ya reli na yale ya bandari, hatukumsikia Rais akizungumzia kuhusu wenyeji kupewa kazi hapo. Twataka katika bandari ya Mombasa wenyeji waweze kupata kazi kwa shauri upanuzi wa bandari utaleta nafasi zaidi. Jambo la uandikishaji watu kazi katika bandari hiyo tunaona kuwa linanyamaziwa kimya. La mwisho ni kuhusu msongamano. Hii reli ya Wachina haianzi sasa katika nchi ya Kenya. Kulikuwa na reli tangu kitambo. Wazo langu nasema makasha yote katika bandari yawe yakitoka moja kwa moja; inafaa yachukuliwe kwa reli mpaka sehemu za Voi ama mbele ya Mariakani. Wenye maroli waanze kuchukulia makasha hayo huko ili wayapeleke Uganda na sehemu nyingine. Hili litakuwa ni jambo la maana."
}