GET /api/v0.1/hansard/entries/535286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 535286,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535286/?format=api",
"text_counter": 210,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "aliomba msamaha na pia akataja tukio moja la mauaji ya Wagalla. Nataka kusema kuwa, Mhe. Rais, katika jambo hili msamaha huu uweze kupatikana kwa njia ya usawa na uweze kuwa ni msamaha kweli ambao umelenga wananchi wa Kenya. Mhe. Rais, ningekuomba kwa unyenyekevu uweze kuhimiza utekelezaji wa Ripoti ya TJRC ambayo inazungumzia ukweli, haki na maridhiano. Mhe. Rais, katika Ripoti hii, kumezungumziwa mambo mengi sana kuhusu haki nyingi sana za kimsingi kwa sababu wakenya wengi wamekuwa wakinyanyaswa. Mbali na Wagalla, pia imezungumzia Molo. Molo kulikuwa na vita vingi vya kikabila. Pia imezungumzia Pwani ambako kulikuwa na vita vya kikabila vya Kayabombo. Tunasema Ripoti hii ya TJRC itekelezwe. Tusilichukulie kwa urahisi jambo la kusema pole, ni viongozi wachache kutoka Afrika ambao wanaweza kusema pole kwa mambo ambayo yalitokea hapo awali. Ningependa kuzungumzia jambo la ukabila ambalo mhe. Rais amelizungumzia kana kwamba ni jambo ambalo linatugawanya sisi wakenya. Nataka kusema kwamba mbali na kuwa katika zile sekta za umma, pia tuangalie katika sekta za kibinafsi. Hii ni kwa sababu bado sekta za kibinafsi zinaangalia mambo kupitia njia za kikabila. Kwa mfano, kuna ndugu zetu katika jamii ya wahindi, hata katika viwanda vyao wanavyotengeza utapata wanaandika watu kutoka jamii ya wahindi pekee na kuwacha watu katika jamii zingine. Kwa hivyo, Mhe. Rais, jambo la ukabila liangalie sekta za umma na pia sekta za kibinafsi. Mhe. Rais pia alizungumzia huduma za mambo ya afya hasa kwa kina mama. Nataka kumwambia kongole alipotoa amri ya kwamba akina mama wasilipishwe hata ndururu wakati wanataka kujifungua. Nataka kuzungumzia jambo ambalo lililetwa na mama yetu Mhe. Margaret Kenyatta, la kutuletea gari lile la ambulance ambalo linasaidia kina mama katika mambo ya uzazi, lakini tunasema tumepatwa na changamoto. Tumeona katika kaunti moja, gari hili limevunjwavunjwa, vifaa vimeibwa na gari hili sasa limekuwa kama gofu. Nasema kwamba wakati mama umetufanyia mradi kama huu tunataka kuwe na njia ya kusimamia mradi huu ili akina mama waweze kupata huduma. Kaunti zinasema hazina mgao wa kutosha na hazina mgao ambao unaweza kutumika katika mradi huu ambao tumeletewa na mama yetu mpendwa, mama Margaret Kenyatta. Kuna ufisadi. Rais amefanya kazi yake. Katika maoni yangu, Tume ya Kupambana na Ufisadi imemwangusha Rais. Lazima tume hiyo ipigwe msasa. Sharti wanatume hao wachunguzwe ili tufahamu kama kweli wanayo tajriba ya kupigana na ufisadi au la. Je, wao ni wanatume wa kiholela? Je, wao ni wanatume ambao badala ya kupigana na ufisadi wanaurejesha kupitia mlango wa nyuma? Baadhi ya wale waliotajwa katika hiyo Ripoti ni Mheshimiwa Keter, Mheshimiwa Birdi na Mheshimiwa Serut. Katika malalamishi yaliyotajwa, hata sisi ambao hatuna---"
}