GET /api/v0.1/hansard/entries/535436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 535436,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535436/?format=api",
"text_counter": 360,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Suala la kuomba msamaha ni suala ambalo linataka mtu ambaye ameheshimu na kuwapenda watu wake. Kuomba kwake msamaha kulikuwa si uoga bali ni upendo na heshima kwa Wakenya wote kwa jumla. Vile vile, tunafahamu kwamba Wakenya wamekuwa wakigawanyika vikundi vikundi kulingana na makabila yao kwa sababu ya matatizo yaliyowakumba kwa miaka mingi. Hivi sasa Rais anataka kuwaweka Wakenya wote pamoja ili awahudumie wakiwa na haki kama wengine wote walio katika nchi hii."
}