GET /api/v0.1/hansard/entries/535440/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 535440,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535440/?format=api",
    "text_counter": 364,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shabaan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Vile vile, ningependa kutoa shukrani kwa Rais kwa sababu alizungumza kuhusu elimu bila malipo sio tu katika shule za msingi bali pia katika shule za upili, ambako wanafunzi wetu watapata elimu bila kulipa karo. Bei ya stima imeshuka. Kushuka kwenyewe kusiwe tu kwa muda mfupi bali Serikali ya Rais Kenyatta iendelee kuhakikisha kuwa bei ya stima inashuka ili watu wote nchini waweze kupata stima. Pia, wawekezaji nchini wawekeze kwa njia rahisi ili bei ya stima isizifanye bidhaa ambazo watakuwa wanatengeza kuwa za bei ya juu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, si siri kuwa shughuli ya mradi wa reli unaendelea. Vile vile, shughuli za ujenzi wa barabara zinaendelea. Mojawapo ni barabara ya kwangu nyumbani, Taveta hadi Mwatate na kuelekea Voi. Hizo ni shughuli ambazo Rais amezitekeleza. Tunafurahi kwamba kazi hiyo inaendelea kote nchini. Rais aliahidi kutengeneza kilomita 10,000 za barabara. Ni kweli kwamba ujenzi wa kilomita 3,000 za mwanzo utaanza hivi karibuni. Huwezi kuzungumzia suala la usalama bila kuzungumzia vijana wetu 10,000 ambao walikuwa wamepewa nafasi ya kupata mafunzo ya kuimarisha usalama. Kama shughuli hiyo haingesimamishwa, hivi sasa tungekuwa tunafanya awamu ya pili – yaani vijana wengine 10,000 wangekuwa wanaajiriwa. Jambo hili limekuwa donda ndugu baada ya korti kuisimamisha shughuli hiyo. Ningependa kuzungumza kuhusu vyeti vya kumiliki ardhi. Serikali hii ya Rais Uhuru Kenyatta tayari imetoa vyeti 400,000 vya kumiliki ardhi. Makadirio yake ni kwamba itatoa vyeti milioni tatu kufikia mwaka wa 2017 ili watu waweze kuwa na vyeti vya kumiliki ardhi na kukaa bila wasiwasi. Nazidi kumpongeza Rais kwa kulizungumzia suala nyeti ambalo limekuwa donda ndugu na kama saratani inayotumaliza humu nchini. Rais alileta kilio. Kilio chenyewe ni kuhusu ufisadi. Rais amekuja kutuomba msaada. Jambo hili lisichukuliwe kama dhihaka The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}