GET /api/v0.1/hansard/entries/535446/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 535446,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535446/?format=api",
    "text_counter": 370,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunihurumia. Nimeshindwa kwenda kula chakula cha mchana ili niwe wa kwanza kuzungumza lakini sikupata nafasi kwa sababu kadi yangu haifanyi kazi. Ninataka pia nichangie kuhusu Hotuba ya Rais. Nitaanzia masuala ya usalama.Ukweli ni kwamba Rais ni mtu mzuri lakini kwa sababu haambiwi ukweli, maneno yanaharibika na watu kila wakati ni kusifu mahali ambapo hapastahili. Usalama umezorota Kenya nzima. Watu wanauawa na wengine wanapata shida. Mpaka hivi sasa njaa imezidi kwa sababu utalii umekufa. Utalii umekufa kwa sababu watalii wanasema Kenya haina usalama. Leo mtu anasimama na kusema kwamba usalama umeimarika kisawasawa. Tafadhalini, nawaomba wabunge na Wakenya wote haswa wale walio karibu na Rais wamweleze maneno ya ukweli ili tuweze kufaulu katika maisha yetu. Usalama si mzuri. Usalama huenda ukazidi kuharibika kwa sababu hali ya unyakuzi wa ardhi umepita kiasi. Kama kule kwangu Matuga, ardhi imenyakuliwa na hata kama tunasema kwamba title deeds zinatolewa, mimi ninasema hata heri zisije kwa sababu ukiangalia waliopata, karibu theluthi moja ya watu sio wenyeji. Katika hali hii, kule kwangu haswa kuna fujo na tunataka Serikali ihakikishe kwamba wanaohusika kupata ardhi ndio wale wenyewe. La si hivyo, usalama utazidi kuzorota kwa sababu watu hawawezi kukubali kunyakuliwa ardhi kiwaziwazi ilhali wanaona. Kwa hivyo, masuala ya usalama hayajakuwa mazuri na lazima Rais aambiwe ukweli ili tuweze kufaulu katika hili suala. Masuala ya pesa za wazee, ninaona hata badala ya pesa za wazee kutujenga sisi, zinatuharibu kwa sababu ndani ya kata moja ambayo ina wazee karibu 200 wanapata wazee 15. Sisi tunajulikana kwamba tunatoa pesa hizo. Sasa, mara kwa mara tunaambiwa tutawaachia watu wenu 15 wawapigie kura kwa sababu wale wazee wengi hawajapata pesa hizo. Ikiwa pesa za wazee zinataka kutujenga sisi basi Rais aongeze pesa hizo kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}