GET /api/v0.1/hansard/entries/535447/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 535447,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535447/?format=api",
"text_counter": 371,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": "wingi ili kila mzee aweze kupata. Hapo majina yatakuwa yamejengeka na mambo yatakuwa yameenda barabara. Bila ya hivyo, tutaendelea kumsifu na hali maneno yanaharibika, sawasawa na kusuka kamba ilhali huku nyuma inachomeka. Mambo mengine ambayo ningependa kuyazungumzia ni mambo ya kutajana katika hizo orodha za wale ambao wamefanya ufisadi. Sijapinga lakini ni lazima kuwe na ushahidi mkali. Kwa wale ambao walikuwa hai zama za akina Njonjo kulikuwa na usaliti. Wakati huo, watu walipata nafasi ya kuanza kuwataja watu wengine ambao walikuwa wapinzani. Tukiendelea katika hali hii, mimi ninaona kwamba hali itakuwa vilevile; watu kutajana, mtu kama anakupinga unamtaja mradi tu wewe uwe karibu na Serikali. Unajitajia yeyote ili mtu aweze kupata shida pengine kwa sababu ni mpinzani wako ambaye unaona kwamba anakupatia taabu. Najua kwamba Rais siye aliyeenda kuangalia yale majina, ni watu wanapeana majina na majina hayo mara nyingi huwa yanaleta shida kwa sababu wale maadui huwa wanataka kuhakikisha kwamba wenzao wamepata shida."
}