GET /api/v0.1/hansard/entries/535448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 535448,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535448/?format=api",
"text_counter": 372,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": "Kwa hivyo masuala ya kutajana ni lazima tuwe waangalifu au sivyo chuki itazidi kuendelea katika nchi hii yetu ya Kenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda, napongeza masuala ya pesa za mashujaa lakini nasema kwamba pesa hizi ni lazima ziongezwe mara kumi ili ziweze kufidia kila shujaa. Mara kwa mara, tunapata mambo kama haya na kwamba kuna watu wanatajwa mashujaa lakini utaona kwamba mashujaa wanatoka sehemu fulani. Kule Pwani, nakumbuka nilipokuwa kijana, hayati Jomo Kenyatta alikuwa akija kule anakaa kwa Mzee Bambaulo, Mzee Mbonze Mbonze au kwa Mzee Mwamgunga. Hawa ni watu ambao walipigania uhuru kikamilifu lakini watu wao hivi sasa wanateseka na orodha ya mashujaa ikiletwa, wao hawamo. Kwa hivyo, hili jambo la kuchagua watu wa sehemu fulani kwamba ati wao ndio walipigania Uhuru, sisi hatuwezi kukubaliana nao. Ikiwa walikuwa wanapigania mashamba yao ni sawa lakini Uhuru ulipiganiwa na Wakenya wote na kwa hivyo mashujaa waangaliwe kutoka kusini mpaka kaskazini; kutoka magharibi mpaka mashariki. La sivyo, hali hii itakuwa haileti maana na ukweli ni kwamba utakuwa ni ubaguzi wa mwaka ambao sisi hatuwezi kukubaliana nao. Mhe. Naibu Spika wa Muda, hiyo ndio hali nilikuwa naifikiria kwamba si hali nzuri. Narudia ya kwamba wale walio karibu na Rais, wamshauri kisawasawa. Mambo ya kuunga mkono lolote linalokuja na japo suala la maana, hayatatusaidia bali yatatutia katika mashimo. Mambo ya kusimama hapa kwamba huyu ni wa muungano wa CORD au Jubilee na sasa lolote baya linalozungumzwa na CORD, mtu wa CORD anaunga mkono, likizungumzwa baya na Jubilee, watu wa Jubilee wanaunga mkono; hatutafika popote isipokuwa tutamaliza nchi hii. Asante sana."
}