GET /api/v0.1/hansard/entries/535505/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 535505,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/535505/?format=api",
"text_counter": 429,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda. Naomba nami nitoe mchango wangu kwa Hotuba ya Rais kuhusu hali halisi ya nchi yetu. Nitazungumzia masuala kadha wa kadha. La kwanza ni uwajibikaji wa wananchi kuhusu usalama. Nakubaliana na Rais kuwa usalama ni jukumu la kila mmoja wetu na lazima tufanye bidii ili tuhakikishe kuwa unaimarishwa. Hata hivyo, naomba pia nitoe maoni yangu kuhusu ugatuzi na jinsi ufisadi unavyoendelea huko mashinani. Tunaulizana ni lipi linaendelea. Rais ametuletea orodha hii hapa Bungeni. Wale Wakristo ambao wako hapa wananisikiza wanajua kwamba wayahudi walipotaka kumsulubisha Yesu walimpeleka kwa Pilato. Pilato aliona mambo ni magumu akanawa mikono yake. Rais ameona hii ni kazi nzito naye amenawa mikono yake na akaitupia Bunge ili lizungumze. La mwisho, lazima EACC ipeleke watu hawa wote kortini ili kila mtu apewe nafasi yake ya kujieleza asije akahukumiwa bila mashtaka. La mwisho ni kwamba ufisadi umekithiri sana na naomba niangazie kwa undani sana. Hata barabara yetu ya kutoka Mwatate kwenda Wundanyi imekwama. Baada ya kandarasi kuwekwa, tunaambiwa kwamba mwenye kandarasi amefilisika. Sababu kuu ni ufisadi ambao ulifanywa na wale wanaohusika na mambo ya kupeana kandarasi za The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}