GET /api/v0.1/hansard/entries/5367/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 5367,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/5367/?format=api",
    "text_counter": 363,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaomba kutoa mchango wangu kuhusu Hoja hii ambayo Bunge linapendekeza. Kama tujuavyo, pahali pa mazoezi na mankuli ni pahali ambapo ni pa muhimu sana kwa Wabunge. Kama hakutakuwa na kamati maalum ya kushughulikia jambo hili, kamati ambayo iko na uzoefu na ambayo inaweza kushughulikia shughuli kama hii kwa undani, hata Bunge lenyewe litafadhaika. Tukiangalia pahali petu pa mazoezi, mpaka sasa haparidhishi. Hapajafikia kile kiwango ambacho tulikuwa tunatarajia kinaweza kuwa kwa Wabunge. Ni muhimu kuwa, wakati huu ambao tunasawazisha mambo mengi nchini, vitendo kama hivi vya pahali pa mazoezi, navyo vipate nafasi ya kusawazishwa, ili navyo viweze kufaa kutoa nafasi ya kutosha ya kupatia Wabunge yale mazoezi ambayo wanahitaji. Ninaunga mkono ombi ambalo lilitolewa na mhe. Khalwale kuwa, ingekuwa jambo la busara kama tungeona Wabunge akina mama wengi katika kamati hii. Lakini hata hivyo, ninaomba niseme kuwa wale ambao wameteuliwa katika kamati hii wajijumuishe kwa kikamilifu ili wahakikishe kuwa, hata chakula kile ambacho tunapatiwa, angalau kiwe na sura ya kiafrika. Tumekula vyakula vingi ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa ni mfano tu. Bado tunakumbushwa ubepari. Nchi hii iko na vyakula vya aina nyingi vya Kiafrika. Tunaomba kamati hii, inapopitishwa ihakikishe kuwa jambo hili linatiliwa mkazo. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}