GET /api/v0.1/hansard/entries/536808/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 536808,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/536808/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Leo ni siku ya maana kwa Seneti hii kwa sababu tunajadiliana pesa zilizotengewa Serikali za Kaunti. Sisi twataka kuupitisha Mswada wa kuzipa pesa Serikali hizi kwa minajili ya maendeleo na kazi zingine za muhimu. Hatupitishi pesa hizi kusudi magavana wa kaunti wajipendekeze kwa wananchi kwamba wao ndio wenye pesa. Kama hawaangalii runinga, waangalie ili waone ni akina nani wanaopendekeza mgao huu wa pesa. Je, ni nani aliye na kibuyu au kifurushi cha pesa? Ni Bunge la Seneti. Wanafaa kwenda nje na kusema; “pesa hizi nimewaletea ni Sen. Machage aliyezitafuta.” Hivi leo twaangaza macho yetu kwa Kshs258 billion ambazo zimegawa na Bunge la Kitaifa. Kuna mgao mdogo kwa minajili ya matibabu ya akina mama, vifaa vya matibabu, kusaidia hospitali za kiwango cha Daraja la 5 na kadhalika. Tunapendekeza kwamba Serikali hizi zipate mgao wa Kshs283,741,685,204. Hizi si pesa chache kwa sababu ukizaliwa leo na uanze kuzihesabu, utafika umri wa miaka 87 kabla kumaliza. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}