GET /api/v0.1/hansard/entries/536810/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 536810,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/536810/?format=api",
"text_counter": 128,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, tulikuwa na shida kwa mgao uliopita. Lazima tuuangalie na kuona tutapeana pesa kiasi kipi katika kila kaunti. Shida tuliyonayo ni ya ufisadi. Tayari, magavana kadhaa wametajwa katika orodha ya ufisadi. Je, tunawapa pesa zaidi ili waendelee na visa vya ufisadi? Na si magavana peke yao, pia Mkaguzi Mkuu wa Serikali ametajwa katika orodha hii. Je, sasa tunawapa pesa zaidi waendelee kuiba? Wamekuwa wezi sugu. Mhe. Rais mwenyewe, katika Hotuba yake, aliukemea ufisadi unaoendelea hapa nchini. Seneti hii iliunga mkono Hotuba yake kwa dhati. Sasa twataka kuona matokeo. Bw. Naibu Spika, tunajua walitajwa lakini tumepata Ripoti ambayo imependekezwa hapa na Mwenyekiti wa hii Kamati kwamba ni zaidi ya kaunti 30 ambazo zimetajwa. Wengine wamekula mpaka wameanzisha vita katika kaunti zao. Mifano mzuri ni kaunti za Narok, Tana River, Kilifi, Migori na kadhalika. Wemekula mpaka wamelewa; wanatapika kila mahali. Lakini sisi kama Seneti tunatekeleza waajibu wetu. Inafaa tuwaambie wananchi wafungue macho yao waangaze akili na mawazo yao vile pesa zao ambazo tunapendekeza leo hii zitatumika mashinani. Inafaa wananchi watambue kwamba hizi ni pesa zao na wala si pesa za gavana, eti ajifurahishe kwa kukimbia kwa magari ya ving’ora kushoto, kulia na kati. Bw. Naibu Spika, hasa hizi pesa Kshs4 bilioni ambazo zimewekwa wakfu kwa sababu ya mambo ya dharura na majanga ambayo yatatokea; pesa hizi zitashughulikia mikasa kadha wa kadha. Kwa mfano shule ikiteketea, janga la kipindupindu kama ilivyo kule Migori na kadahalika---. Wakati jambo la dharura litatokea, gavana watajingamba kwa kupeleka kule hizi pesa na kudanganya wananchi kwamba wao ndio wamezitoa ilhali sisi ndio tunazipitisha hapa. Hizi ni hela za kuwasaidia wananchi hasa wakati wa majanga mashinani. Kwa hivyo, hatutaki kusikia kwamba mwananchi anaumiwa huku kuna pesa ambazo tunapitisha hapa. Haifai kumpigia magoti gavana, kumhusudu na kumuita majina ya enzi au ya kifahari ili afurahi naweze kuwarushia pesa chache kwa minajili ya janga litakalotokea mashinani. Inafaa wananchi wajue kwamba hii ni haki yao. Ni lazima kuundwa kamati ya majanga mashinani. Tutapitisha hizi pesa, lakini usimamizi wake usiwe kitendawili ambacho kinaweza kutatuliwa tu na magavana. Hata kama Katiba inawapa magavana uwezo wa kugawa pesa hizi ni lazima wawe waangalivu. Ombi letu kwao n waache uchoyo na kujitukuza. Sen. (Dkt.) Khalwale amesema kwamba vifaa vimetolewa na Serikali. Hata hiyo, pesa hazijatolewa kwa minajili ya kuanzisha mipango ya kujenga maharaba. Inafaa hili jambo liangaliwe kwa undani kwa sababu itakuwa ni aibu kama vifaa vitatolewa na Serikali kuu kwenda mashinani halafu visifanye kazi. Kwa hivyo, ni lazima tujenge mahabara na kuyapea vifaa. Mimi ni daktari na ninajua umuhimu wa hili jambo. Ni lazima hawa magavana waweke sahihi kwa vile vipengee vitatu ambavyo hawakutia sahihi ili mpango huu ukamilike. Ninashukuru kwamba Serikali kuu imekubali kutoa hizi pesa. Tulikuwa tunafikiria kwamba watatoa vifaa mashinani halafu wakaingiza kwa mfuko. Ninashukuru kwa sababu wamefanya jambo la utu na la maana ili kuhakisha kwamba hizi pesa zimetoka kwa Serikali kuu. Pia kuna pesa za ziada ambazo zitatolewa kwa zile sehemu ambazo labda maendeleo hayakufika. Ni lazima tuangalie mambo haya kwa sababu mgao wa hizi pesa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}