GET /api/v0.1/hansard/entries/536837/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 536837,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/536837/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili kwa roho ngumu na huzuni mwingi niunge mkono Mswada huu. Kama ningekuwa ni mtu wa kawaida ningeupinga Mswada huu lakini kwa sababu mimi ni Seneta, nitaunga mkono. Nitatoa sababu kwa nini naunga mkono Mswada huu. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu tunaongeza pesa kwenda katika serikali za kaunti. Je, serikali hizi za kaunti zinajua kama sisi tunafanya kazi hiyo? Hao magavana wanajua na kuheshimu Seneti kwamba sisi ndio baba na mama wanaowapelekea pesa hizo? Leo hii hapa tunang’ang’ana kuongeza zaidi ya Kshs30 billion lakini ukifika huko, Maseneta hawajulikani wala hawaonekani mahali popote. Hakuna mahali ambapo Seneti inasemekana kwamba imefanya kazi hii. Hii imekuwa kama hadithi ya mnyama fulani kufukuza mnyama na akishamshika, anapewa mifupa. Sisi kazi yetu hatueleweki wala hakuna jambo lolote tunalolifanya katika kaunti zetu. Ikizidi, wanasema kwamba Maseneta wako Nairobi na kazi yao ni kula chapati na kuku na wala hatufanyi kazi. Wakati huu haya ndio mambo ambayo tunatetea na tunataka pesa nyingi kwenda katika kaunti kwa sababu ya kufanya mambo ambayo yatakuwa na manufaa ya watu wetu. Kwa mfano, kuna pesa za dharura. Ni nani asiyekubali kwamba kaunti zetu zote zina mambo ya dharura. Kuna dharura za ukame, vyakula na kadhalika. Ndio maana kifungu hiki cha pesa za dharura ambazo zimetengwa na Seneti hii, naishukuru sana Kamati ya Fedha na Bajeti kwa kutenga fedha za dharura katika kaunti. Tukiangalia fedha za afya ni kwamba Kamati ya Fedha na Bajeti yataka kuona kwamba wananchi katika kaunti wanapata huduma nzuri za afya. Jiulize ni hospitali gani katika kaunti utapata ina madawa na vifaa vya kutosha? Hali ni ile ya miaka nenda, miaka rudi na hakuna mabadiliko. Haya ndio mambo ambayo tunasema tuna uzitu mkubwa wa kuongeza pesa hizi. Tunachohitaji zaidi ni kuonekana ya kwamba kuna mambo yanayobadilika katika kaunti. Hali za wananchi wetu bado ni hali zile za “19 vua” kofia mpaka leo. Hakuna madadiliko hospitalini; foleni ni zile zile, shida ni zile zile. Sasa imekuwa ni hatari bin danger ."
}