GET /api/v0.1/hansard/entries/536894/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 536894,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/536894/?format=api",
    "text_counter": 212,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Kwanza, leo ni siku kuu katika Kenya nzima. Nataka magavana na waaakilishi wa wadi kujua kwamba Maseneta ndio wanaogawa pesa. Pesa hazitoki kwa magavana. Pesa zinatoka kwa Maseneta. Sisi ndio tunaogawa pesa. Leo, nataka wanisikilize vizuri. Pesa wanazozitumia kwenda safari za ulaya na kule kwingine ni sisi ambao tunazipitisha ili kufanikisha maendeleo. Wakenya walipitisha Katiba mpya katika mwaka wa 2010 na wakasema wanataka ugatuzi kwa nia moja na sababu moja ya kuleta maendeleo. Miaka miwili tangu tuje hapa, hakuna maendeleo yanayoonekana mashinani. Hii ni aibu kubwa. Kwa hivyo, tungependa kuwaambia magava na waakilishi wa wadi kwamba pesa tunazotaka kuwaongezea leo si za kwenda safari ama kununua magari makubwa. Hizi ni pesa za kujenga kaunti ili tuwe na maendeleo. Nataka kuona barabara nzuri, watu wangu wakiwa na maji safi na hospitali zetu zikiwa na madawa na vifaa vingine. Hivyo ndivyo tutakapofurahia ugatuzi. Kwa sasa, wengi tunalia. Wanaochomoa vitambi wakijidai wao ndio wanaofanya kazi bora katika Serikali za kaunti lakini mwananchi analia. Magavana 13 wanasemekana wako katika orodha ya wale waliopora pesa za wananchi. Leo, tunawaongezea pesa lakini tunataka kuwaonya kwamba pesa hizo ni za maendeleo na si kutumika kununua magari au kwenda ulaya ama kuwahonga wapinzani wao. Leo nataka kazi ya Seneta ijulikane. Nitaenda kwetu nisema kufikia leo, nimepeleka Kshs8 billion lakini hakuna chochote kinachoonekana pale mtaani kwa sababu waakilishi wa wadi na magavana wanaenda safari na kutumia pesa vibaya. Pesa tunazowaongezea leo zinafaa kuonyesha ugatuzi. Zile pesa ambazo tunapewa za uchunguzi Kshs1 billion na kuona pesa zimetekelezwa zitatufaa sana. Tutaleta ripoti hapa kuonyesha pesa ambazo zimetumiwa vibaya. Wakizitumia pesa vibaya, tutaleta Hoja hapa ya kuwaondoa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}