GET /api/v0.1/hansard/entries/536896/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 536896,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/536896/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "magavana hao kabla ya mwaka 2017. Hii ni kwa sababu Katiba yakubali sisi tufanye hivyo. Jambo la tatu ni kwamba pesa tunazoomba ziongezewe hazifai kuombwa. Pesa za majanga ni lazima ziende mahali majanga yanapotokea na hapo ni katika makaunti. Pesa za mishahara, hata kama kila mwaka kuna nyongeza ya mishahara, hiyo ni haki ya kibinadamu. Hatuombi pesa hizi. Ni lazima zipeanwe. Kitu tunachoomba ni kwamba pesa zikienenda katika kaunti, zinafaa kugawa kinaga ubaga. Tunafaa kujua kiwango cha county assembly ni kipi na pia za Executive ni ngapi na za maendeleo ni ngapi. Wananchi wanafaa kujua. Ni haki yao kuuliza mbona hakuna maendeleo. Hatufai kungoja mpaka 2017 ili watu waondolewe. Tunataka wakati huu, watu waajibike. Twataka waajibike. Wale ambao wametajwa katika orodha ya kupora wananchi nasikitika kwa sababu ni lazima kwanza wapelekwe kortini. Kama Gavana wangu angetajwa, ningekuwa wa kwanza kumtoa ofisi. Ni aibu kuona Gavana anakataa kusimama kando na huko amepora pesa za wananchi. Kama angetajwa Gavana wangu, ningekuwa wa kwanza kumtoa ofisi. Wacha pesa hizi zipelekwe katika kaunti. Tulipitisha pesa hizi si kutajirisha mtu mmoja lakini kuleta maendeleo katika kaunti."
}