GET /api/v0.1/hansard/entries/536903/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 536903,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/536903/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mara nyingi tumeona Maseneta wakienda mahali, utakuta ya kwamba Seneta hatambuliwi kwa sababu wakati wa kutoa pesa, maseneta wengi huwa wamepungukiwa. Kwa hivyo, inafaa pesa hizi zitumiwe kwa ukadirifu. Inafaa pasa hizi zitumiwe vizuri. Hivi juzi hata mhe. Rais Uhuru Kenyatta alisema kwamba kuna magavana fulani ambao wametumia pesa vibaya. Kweli ni ubinadamu kwa mtu kutenda kitendo kama hicho. Lakini tunasema kwamba ikiwa jambo kama hilo liko, basi ingekuwa vizuri kama wangejiondoa ili uchunguzi ufanywe. Ikipatikana kwamba hawana makosa yoyote warudishwe kwa kazi zao kwa sababu hizi pesa tunapeleka katika kaunti ni nyingi sana na tunataka uangalifu. Tumeongezea pesa za mahospitali, barabara na hata kuongeza mishahara yao. Kwa hivyo, mambo ya matumizi ya pesa yanataka uangalifu zaidi. Watu ambao wamekadiriwa uwezo wa kutumia pesa inafaa wazitumie kwa hali ambayo wananchi wa Kenya wataona maendeleo katika serikali zao za mashinani. Bw. Spika wa Muda, sisi katika Seneti hatutakubali pesa ambazo zinapelekwa mashinani zitumiwe vibaya. Ikiwa zitatumiwa vibaya, basi hatua ya kisheria ni lazima ichukuliwe. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu."
}