GET /api/v0.1/hansard/entries/536960/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 536960,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/536960/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Hassan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 431,
        "legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
        "slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Mswada huu na Ripoti hii ya Kamati ya Finance, Commerce and Budget. Mengi yamesemwa na wenzangu, lakini ninaunga mkono na kujishirikisha na maoni yaliyotolewa na Sen. Wetangula na Sen. Muthama. Lakini katika yote haya, nimesikia wengi wakisema kwamba tunazipeleka fedha kwa magavana. Magavana hawa hawataki kuwajibika kwa mtu yeyote. Labda sisi tuna viungo spesheli ambavyo tumepewa na Mwenyezi Mungu ambavyo vinafanya tupitishe sheria ambayo inawafanya wawajibike mbinguni peke yake. Magavana hawa hawataki kuwajibika kwa Seneti, hawataki kuwajibika kwa Tume ya Ufisadi au kwa mtu yeyote. Wanataka kupelekewa neema ili watumie. Labda wangependa tusema kwamba kwa sababu wao ni waokozi wetu, basi tunafaa kuwapa nafasi ili wasiajibike kwa njia yoyote. Mahali wametufikisha hawaamini kwamba wanaweza kuwajibika kwa mtu yeyote. Mimi ningependa kuunga mkono Mswada huu, lakini inafaa tuzingatie swala la magavana kuwajibika. Kama hawataki kuwajibika kwetu, viumbe, basi wanafaa kuwajibika kwa Mwenyezi Mungu. Watu hawa 47 wako katika tabaka lao. Wanataka kupewa pesa na kufanya kazi. Leo tunapigana hapa kuhakikisha kaunti zetu zimepata pesa. Tunapoenda katika kaunti, wanatudharau na kutufanyia mambo mengi na kutuonyesha kwamba wao ndio wafalme na wakubwa; wao ndio watawala. Kama wanataka utawala, basi waje hapa ili wapitishe kanuni za pesa. Mimi hapa na wenzangu tunajaribu ili tupate kiwango kikubwa cha pesa kuwafadhili."
}