GET /api/v0.1/hansard/entries/537179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 537179,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/537179/?format=api",
    "text_counter": 497,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, nipe nafasi niseme haya. Kila mtu akianza kulia, wengine wako na sauti kubwa kuliko wengine. Lakini sio kwamba wengine hawana uchungu. Wengine hulia kimoyomoyo, lakini wote huwa wanalia. Wote tuko na shida hiyo. Katika Kaunti ya Migori, tunakodesha nyumba. Naibu governor alifukuzwa kutoka kwa ofisi ya serikali kwa sababu ni hiyo serikali ya Jubilee imekata kuonga Katiba yasema nini kwamba tuwe na serikali moja mashinani. Wamesema kwamba lazima serikali za provincial administration ziwepo. Basi mle hayo machungu. Isingekuwa hivyo basi tungewawia radhi na kuwapa nafasi hawa wenzetu wapate wanayoomba. Wote tuko kwa kikapu hicho na yafaa tuwe na Mswada mpya kwamba makao makuu yajengwe. Tupitishe hilo ili sisi wote tupate bahati. Lakini vile ilivyo, watu wane wanaomba na sisi wengine mnataka kutuangusha kura twende nyumbani. Hatuwezi kukubali nzi akidoea na kutumbukia ndani ya mchuzi wetu. Nakataa katakata!"
}