GET /api/v0.1/hansard/entries/537182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 537182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/537182/?format=api",
"text_counter": 500,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Bule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1029,
"legal_name": "Ali Abdi Bule",
"slug": "ali-abdi-bule"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Eneo la Tana River lilikuwa limesahulika kwa miaka nyingi. Lakini leo wakati kuna pendekezo la Tana River kusaidiwa, je, kwa nini sasa Wakenya wasiwe na huruma kwetu? Naomba Maseneta wenzangu waangalie masilahi ya wengine. Sala wa Bwana inasema: “Mtakie mwenzako lile unalojitakia nafsi yako.” Wengine wamebarikiwa na maendeleo. Je, ukiamua leo kwamba sisi pia tujengewe nyumba kisha tujenge yako kesho, kuna shida? Nawaomba wenzangu kwamba mimi ni mmoja wenu. Naomba tupewe pesa hizo leo ili mpate kura yangu. Asante."
}