GET /api/v0.1/hansard/entries/539370/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 539370,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/539370/?format=api",
"text_counter": 19,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Nikikumbuka vyema, kuna wakati ambapo kulikuwa na mapinduzi ya Serikali kwa masaa machache mnamo mwaka wa 1982. Wale ambao walishikwa walisomewa mashtaka na kuambiwa wayajibu. Walidhani waliyajibu mashtaka hayo sawa lakini walishtukia wameyajibu visivyo kwa kudai kwamba hawakuhusika wala hawakiri mashtaka yote. Mmoja wa watuhumiwa hao alisema: “ I am not guilty of all those ”. Hii ina maana kwamba siyo yote anayoyakiri lakini baadhi ya hayo anayakiri. Hiyo ni hali ya kwamba hakuwa anaelewa ni nini kilichomkabidhi hapo mahakamani. Hivyo basi kuna madhara mengi ambayo wananchi wa Jamhuri ya Kenya wanayapata---"
}