GET /api/v0.1/hansard/entries/539375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 539375,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/539375/?format=api",
"text_counter": 24,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwashetani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii ya leo ambayo inaomba kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya muda mrefu sana. Imetokana na shughuli zilizokuwa zikiendelea wakati tulipokuwa tukitafuta hali ya kufanya biashara katika mabandari yetu ya Afrika Mashariki. Kiswahili ni mseto wa lugha tofauti kimaneno. Imechangiwa na lugha kama Kihindi, Kireno na Kijerumani. Ukiangalia yale maneno ambayo yako katika lugha ya Kiswahili, ni lugha ambayo imechanganyisha makabila mengi ya Kibantu. Karibu asilimia 70 ya Wakenya wanaielewa lugha ya Kiswahili vyema. Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Joyce Lay inalenga kutafsiri Katiba ili ieleweke na wananchi. Katiba ni muhimu katika mwongozo wetu wa kukaa salama na kuongozana kwa njia sawa. Kwa upande wa sheria, watu wetu, haswa wale tunaowakilisha, wamekuwa na matata sana wakati wana kesi kortini kwa sababu wakati hukumu inatolewa, wale wanaofuatiliza kesi hizo hawazielewi. Hukumu zote ambazo nimeshuhudia zinatolewa kwa lugha ya Kiingereza, ambayo ina utata sana. Kwa upande wa mahojiano katika kutafuta kazi, watoto wetu wengi wana stakabadhi na wamesoma. Lakini kwa sababu ya kutoweza kujieleza kwa lugha ya Kiingereza kwa sababu ya sehemu wanazotoka ama wanazokaa, inakuwa vigumu wakati The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}