GET /api/v0.1/hansard/entries/540602/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 540602,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/540602/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Shukrani Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Nampongeza sana Mhe. Millie kwa kuwa ameweza kuona yale ambayo yanawakumba akina mama haswa wale ambao tunawaita akina mama tasa. Kusema ukweli, ninazungumza nikiwa mambo haya yalinikumba kupitia kwa mamangu nikiwa mimi ni mtoto wa pekee kwa mama. Niliona jinsi ambavyo mamangu alikuwa anasikitika kwa kuwa alinizaa peke yangu na hakuweza kupata watoto wengine hadi ikafikia kiwango cha kumlazimisha babangu aoe mke mwingine ili aweze kupata watoto na kuwaita watoto wake naye pia. Lakini basi, ikiwa tunaunga mkono huu Mswada, ni lazima tuangalie sheria kwa makini haswa zile ambazo zitaweza kulinda huyu mtoto atakayezaliwa na mama atakaye kuwa amebeba hiyo mimba inayotokana na mbegu ya mtu mwingine. Tusije kufungua njia ya kuwasaidia wale ambao wameamua kuishi kinyume na maadili ya kibinadamu, kinyume na maadili ya dini na nikizungumzia hususan wale ambao tunawaita kwa lugha ya Kimombo gays na wanawake lesbians . Kwa Kiswahili wale wanawake huitwa msago. Tusipokuwa na umakini wa sheria, tutawafanya hawa watu kuendeleza hizo tabia zao wakijua kwamba hata mtu asipozaa, ana njia ya kupata mtoto na kudai kuwa yule mtoto ni wake. Hii itakuwa imewapa nafasi wale ambao wanataka kuendeleza uchafu huo kuwa wanaweza kuuendeleza na itaambukiza vizazi vingine. Hivyo basi nikiunga mkono sheria hii, nampongeza Mhe. Nyikal kwa kutufafanulia zaidi akiwa yeye ni daktari anayeelewa zaidi mambo yanayohusiana na uzazi kupitia teknolojia mpya ambayo tumeweza kuirithi katika ulimwengu huu wa sasa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}