GET /api/v0.1/hansard/entries/540603/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 540603,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/540603/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Katika hali ya kupongeza, ningependa pia tuweze kuelewa ya kwamba tutakuwa tumempa mtoto huyu ulimwengu, lakini je, mtoto huyu atakuwa mwenyewe ni nani? Ataweza kupata haki zake kama mtoto kwa nani? Kwa sababu atakuwa haelewi babake na mamake ni yupi kwa sababu anaambiwa wewe ulizaliwa kupitia mbegu zetu na yule ambaye alimbeba kwa miezi tisa atasema mtoto ni wake. Mwishowe, yule mtoto ataishi katika maisha ambayo hajielewi, maisha yake iko mikononi mwa nani? Pia tuweze kuangalia kuwa kuna wale ambao watajitolea kutoa mbegu zao na baadaye aje aone kwamba hana haja tena ya kuweza kuwa na yule mtoto. Je, na yule aliyebebeshwa ule mzigo, ni nani atakayemtunza mpaka atakapozaa yule mtoto? Kwa sababu atakuwa anahitaji kulewa ndio yule mtoto aliye tumboni aweze kukua na aweze kuzaliwa. Katika sheria ambazo tutaweza kuangalia katika Bunge hili ambayo nina imani kuwa vichwa vilivyoko hapa ni vichwa ambavyo vinaelewa kila neno kwa ufasaha, tutaweza kutoka na mwelekeo ambao utaweza kusaidia jamii kwa vizazi vijavyo bila kuhitilafiana na dini na bila kuhitilafiana na maadili yetu ya utamaduni wetu. Naomba kukomea hapo. Ninapongeza na hii sheria tuiendeleze tuweze kuchambua zaidi na tupate kitu mwafaka ambacho kitasimamia hili neno bila kuleta utata kati yetu binadamu."
}