GET /api/v0.1/hansard/entries/541217/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 541217,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/541217/?format=api",
"text_counter": 35,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika. Naunga mkono ombi hili kama alivyozungumza Mheshimiwa. Jana tulizungumzia mambo ya ufisadi na tukachukua hatua kulingana na sheria vile ambavyo imetupatia uwezo. Lakini huu usiwe ndio mwanzo ama isiwe ndio tumeishia hapo kwa sababu ukiangalia matatizo yalio katika barabara zetu hususan barabara ya Mombasa, Eldoret mpaka kuvuka mpaka Uganda, barabara zimeharibika vibaya sana. Zimeharibika kwa sababu magari yanabeba uzani zaidi ya vile inatakikana. Unashangaa hivi vituo vya kupima uzani viko katika maeneo mbalimbali, mbona barabara ziharibike na yale magari hupita pale? Inamaanisha kuna mengi ambayo yanafanyika katika vile vituo vya kupima uzani na hakuna hatua inayochukuliwa. Sijui kama tunaweza kupendekeza kupitia hapa kwamba pengine wale maafisa wote wanaosimamia vituo hivyo waondolewe tuweke watu wapya na tuanze kuwachunguza sawasawa. Hiyo inaweza kutusaidia wakati huu."
}